Home Kitaifa MUWASA KUITUMIA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KURUDISHA MAJI KWA WALIOSITISHIWA BILA...

MUWASA KUITUMIA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KURUDISHA MAJI KWA WALIOSITISHIWA BILA FAINI

Na Shomari Binda-Musoma

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) inaitumia wiki ya Huduma kwa wateja kurudisha huduma ya maji kwa waliositishiwa kwa muda mrefu.

Huduma ya matumizi ya maji itarejeshwa kwa wateja hao bila kulipia faini ambayo inapaswa kulipiwa baada ya kusitishiwa.

Akizungumza na Mzawa Blog mkurugenzi wa MUWASA, Nicas Mugisha amesema maji ni huduma muhimu hususani majumbani na katika kutambua hilo wameamua kutumia wiki ya huduma kwa wateja kutoa nafuu kwa wananchi.

Amesema ili kuwafikia wateja karibu wiki hii wameweka vituo karibu na wananchi kwenye maeneo yao ili kuweza kuwahudumia zaidi.

Nicas wateja ambao wamesitishiwa huduma ya kupata maji wanapaswa kuitumia fursa hiyo kurejesha maji na kuendelea kupata huduma.

“MUWASA tunaitumia wiki ya huduma kwa wateja pamija na mambo mengine kuwarejeshea huduma wateja waliositishiwa bila kulipia faini”

“Tumeweka vituo vya kutoa huduma maeneo mbalimbali karibu na wateja ili kuweza kuwahudumia na tunawaomba wananchi waitumie fursa hii” amesema Nicas.

Mkurugenzi huyo wa MUWASA amesema bado wanaendelea kuwaunganishia wateja wapya huduma ya maji katika maeneo mbalimbali.

Amesema wateja wapya wanaotaka kuunganishiwa huduma ya maji wanaweza kufika kwenye vituo vilivyotengwa kwaajili ya kutoa huduma au ofisi za MUWASA ili kuweza kuhudumiwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!