Na Magrethy Katengu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Slaa amemuagiza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo pamoja na Watendaji wake kushughukia kero ya Urasmishaji wa ardhi inayowakumba wananchi wa Mkoa huo ndani ya siku Saba Kisha wamletee mrejesho.
Agizo hilo amelitoa Leo jijini Dar es salaa wakati alipokutana na Wataalamu wa Ardhi, Viongozi wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam, wataalamu wa ardhi kutoka halamshauri za Mkoa huo,kwa lengo la kujadili namna ya kuondoa kero ya urasmishaji wa ardhi unaofanywa na baadhi ya makampuni binafsi ambayo yanakusanya fedha kutoka kwa wananchi huku yakishindwa kutekeleza majukumu yake.
”Nimechoka kila siku kero kubwa ni ardhi natoa muda wa siku saba kwa watendaji wa Wizara ya Ardhi kuhakikisha wanatatua kero hiyo na baada ya hapo wanirejeshee majibu kwa viongozi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Dar es salaam” amesema Waziri
“Natoa maelekezo yangu kero ya Urasmishaji ni kubwa ,Naibu katibu Mkuu na Watendaji wenzako tukitoka hapa kwenye kikao mkaanze kushughulikia kero hizi ndani ya siku saba ,mlete taarifa kwa viongozi wa chama,kama kuna tatizo la fedha niambie ili tuone tunapata wapi fedha ili muweze kukamilisha kazi hii” amesema
Waziri Slaa amesisitiza kuwa hataki kuskia kero za urasmishaji wa ardhi zinaendelea kujitokeza katika uongozi wake na makampuni yanayojihusisha na urasmishaji huo yanapaswa kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na yale yatakayoenda kinyume yachukuliwa hatua za kisheria .
“Serikali imepanga kupima na kutoa hati za ardhi milioni mbili na laki tano(2.5 milioni) kufikia 2025,hivyo lengo la serikali ni kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi,kwasasa mikoa yote ishirini na sita(mikoa 26) nchini kuna makamishna wa ardhi wanaotoa hati ,hatua hii inasaidia wananchi kupata hati zao bila usumbufu” amesema
Nakuongeza kwamba “Urasmishaji umekua tatizo kubwa katika simu kumi ninazopigiwa na wananchi simu saba hadi nane zinahusu malalamiko ya urasmishaji wa ardhi,sasa hapa nimekuja na timu yangu inayohusika na mambo ya ardhi napenda kuagiza kuhakikisha kero hizi zinashughulikiwa haraka sana acheni kukaa maofisini “.
Awali akizungumza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam Abass Mtemvu amesema kwamba Mkoa wa Dar es salaam umekua na tatizo la urasmishaji kutokana na kazi hizo kupewa makampuni binafsi ambayo yanakusanya fedha za wananchi nakutokomea nazo bila kufanya kazi hiyo kwa wakati.
Amesema kuwa kutokana na tatizo hili kuwa kubwa tumeona tukuite mheshimiwa Waziri wa Ardha najua hata wewe kwenye jimbo lako la Ukonga tatizo hili lipo,nakuomba uzungumze na madiwani,wakuu wa wiliaya na wataalamu wa arfhi madiwani, wabunge na mameya wa waliopo hapa tupo tayari kupokea maelekezo yako ili kuondoa tatizo hili ” amesema Mtemvu mbele ya Mkutano huo.