Na Shomari Binda-Musoma
WANANCHI was Kijiji cha Musanja Kitongoji cha Gomora wameendelea na ujenzi wa madarasa ya shule shikizi ili kuwasaidia wanafunzi wa Kitongoji hicho kutembea umbali mrefu kwenda masomoni.
Kitongoji cha Gomora ni moja ya vitongoji vitatu (3) vya Kijiji cha Musanja, Kata ya Musanja ambacho hakina shule ya msingi kwa sasa.
Vitongoji hivi vitatu (3) vinayo shule ya msingi moja iliyojengwa mwaka 1959 na Kanisa la Mennonite shule hiyo ya msingi kwa sasa ni shule ya serikali.
Matatizo makubwa yanayoikabili kwa sasa shule hiyo ni kutembea kwa umbali mrefu wanafunzi,mrudikano wa wanafunzi madarasani pamoja na uchakavu wa majengo.
Ujenzi wa awali umekamalisha vyumba viwili vya madarasa, ofisi moja ya walimu na choo chenye matundu 6.
Harambee iliyoendeshwa na mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini, kwa kushirikiana na Kamati ya Siasa ya Wilaya (CCM) iliyopigwa likuwa ya mafanikio ya kuridhisa
Kwenye harambee mifuko ya saruji 150, ikiwemo 100 ya Mbunge wa Jimbo na 10 ya Diwani
shilingi milioni 3 za Halmashauri fedha taslimu shilingi 306,000 zikiwemo shilingi 105,000 za Walimu Makada wa CCM, Mchanga tripu 3 zilipatikana.
Wananchi wa Kitongoji cha Gomora waliahidi kuanza ujenzi haraka na kweli wamefanya hivyo .