Na Shomari Binda
WAJUMBE wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamehudhuria kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar na kupata mafunzo.
Ugeni huo visiwani humo ni muendelezo wa ziara ya wajumbe wa UWT wilaya za mkoa wa Mara inayoratibiwa na mbunge wa viti maalumu Agness Marwa.
Wakiwa kwenye kikao hicho cha baraza la Wawakilishi wajumbe hao wamejifunza na kuona namnac vikao vinavyoendeshwa.
Safari hiyo iliyopewa jina la Mara To Zanzibar Royal Tour iliyoandaliwa na mbunge huyo kwa lengo la kuitangaza Tanzania na kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan lakini pia kudumisha Muungano.
Wakiwa Wameongozana na Katibu wa UWT mkoa wa Mara Mariam Kireti,Katibu wa UWT na viongozi wengine wa wilaya ya serengeti wamepata fursa ya kushiriki kikao cha Baraza na baada ya kikao wakapata nafasi ya kuseminishwa juu ya majukumu ya Baraza na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi mheshimiwa Mgeni Hassan Juma ambae amewafafanulia kuwa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ni bunge la umoja wa kitaifa la visiwa vya Zanzibar hivyo linafanya kazi sawa na kwa ushirikiano na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Kwa upande wake mbunge Agnes Marwa ametumia fursa hiyo kumpongeza Spika na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi kwa ushirikiano na fursa waliyotoa, lakini pia amemshukuru na kumpongeza Rais wa Zanzibar Dr. Hussein Mwinyi na serikali yake kwa ushirikiano mkubwa wanaotoa toka ziara hiyo imeanza.
Amesemaa hiyo inaashiria mshikamano na uimara wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
“Nishukuru sana mheshimiwa Spika na Naibu Spika kwa kupata fursa.ya kukaribishwa kwenye kikao cha baraza la.wawakilishi na kuweza kujifunza” amesema Agness.
Wajumbe wa UWT wilaya ya Serengeti wamemshukuru mbunge huyo kwa kuwawezesha kufika visiwani humo na kuweza kujifunza.