Na Shafii Mohammed, TANGA
Maonyesho ya Biashara yanayoshirikisha Wanawake Wajasiriamali maarufu Tanga Woman Gala msimu wa sita yamezinduliwa rasmi ambapo zaidi ya Wafanyabiashara 100 kutoka maeneo Mbalimbali nchini wamepata fursa ya kuonyesha Bidhaa zao ,
Maonyesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi International.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Five Brothers ambao ndio waandaji wa Maonyesho hayo Nassor Makau aliwaambia Waandishi wa Habari mapema Jana jioni kuwa Maonyesho hayo yanatarajiwa yameanza Septemba 28 na yanatarajiwa kufungwa Septemba 30 ,
“Maonyesho haya msimu wa sita yameleta mageuzi makubwa kutokana na wingi wa washiriki kuongezeka zaidi lakini pia tumefurahi kuona kuwa Maonyesho yetu yameleta mageuzi makubwa kwa Jamii kutokana na Wanawake Wajasiriamali kupata mafunzo maalumu ya namna ya kupata mitaji na kuendesha Biashara ,hii imetupa nguvu kubwa ya kuongeza uwekezaji mkubwa wa Maonyesho haya” alisisitiza Makau
Alisema Maonyesho hayo yanaenda sambamba na mafunzo maalumu ya Ujasiriamali kwa washiriki, Maonyesho ya michezo na Utamaduni wa vyakula,
“Maonyesho hayo yanaenda sambamba na mafunzo maalumu ya Ujasiriamali kwa washiriki wetu na pia tuna Michezo Mbalimbali na Utamaduni wa vyakula” alisema
Aliwataka Wanawake kuchangamkia fursa hiyo ili kukuza Biashara zao ,
“Niwaombe akinamama changamkieni fursa hii ili mkuze Biashara zenu lakini pia familia ziwaunge mkono wanawake hasa kwenye masuala mazima ya Ujasiriamali ” alisema Makau
Mwisho