Na Shomari Binda-Musoma
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mara Patrick Chandi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye fainali ya mashindano ya Mathayo Cup jumamosi septemba 30.
Licha ya Chandi fainali hiyo itakayoanza saa 5 asubuhi kwa michezo mbalimbali ukiwemo mchezo wa mashabiki maveteran kuanzia miaka 35 wa Simba na Yanga utahudhuliwa pia na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Musoma mjini Benedict Magiri.
Timu zilizofanikiwa kuingia fainali ya mashindano hayo ni Mwigobero na Nyamatare kati ya timu 16 zilizoshiriki.
Bingwa wa mashindano hayo ataibuka na zawadi ya ng’ombe mkubwa na kombe,mshindi wa pili laki 5 na mbuzi wawili huku mshindi wa 3 akichomoza na shilingi laki 3 pamoja na mbuzi.
Aidha kutakuwa na zawadi za washindi mbalimbali ambazo ximeandaliwa na muandaji wa mashindano hayo mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo.
Katibu wa mbunge Christopher Majala amesema maandslizi yote kuelekea fainali hiyo yamekamilika ikiwemo zawadi kwa washindi.
Amesema wamemualika Mwenyekiti wa CCM mkoa ili kujionea utekelezaji wa ilani ya chama kupitia michezo inavyotekelezwa jimbo la Musoma mjini.
Amesema licha ya kiongozi huyo watakuwepo pia viongozi mbalimbali na wananchi ambao wametangaziwa kujitokeza kwa wingi kuona burudani zilizoandaliwa.
MÃ shindano hayo ya Mathayo Cup 2023 yaliyoanza mwezi uliopita yamekuwa yakihudhuliwa na watu wengi na kufurahiwa huku mashabiki wskiomba kuwa endelevu.