Afisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni ( BRELA ) Vincent Nyanje ( kulia ) akimkabidhi cheti Cha usajili wa jina la Biashara Mkazi wa Mwanza Mhandisi Peter Mbawala ( kushoto ) katika Banda la BRELA kwenye Maonesho ya Sita ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya EPZA Halmashauri ya Mji wa Geita .
Afisa BRELA Anyelwisye Mwakibinga akimsainisha mteja wake Mhandisi Peter Mbawala ( kulia ) mara baada ya kupokea cheti Cha usajili wa jina la Biashara , kushoto ni Afisa Habari wa BRELA Christina Njovu wakiendelea kutoa huduma katika Maonyesho hayo Mjini Geita.
Mkuu wa Sehemu ya Majina ya Biashara BRELA Bw. Harvey Godwin Kombe ( kushoto) akizungumza na wateja wake waliotembelea banda la BRELA kufahamu huduma mbalimbali zitolewazo na BRELA katika Maonesho ya Sita ya Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya EPZA Halmashauri ya Mji wa Geita