Na Shomari Binda-Musoma
WANANCHI wa kisiwa cha Rukuba kilichopo jimbo la Musoma vijijini wameishukuru serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuanza kutoa vifaa tiba kwenye kituo cha afya cha kisiwa hicho.
Wakizungumza kisiwani hapo wananchi hao wamesema sasa wanaanza kuiona neema ya kupata huduma bora za afya wakiwa kisiwani hapo.
Wamesema kwa kuwa wapo kisiwani wamekuwa wakipata changamoto za matibabu rakini sasa changamoto hiyo inakwenda kuisha.
Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Musa Maijo amesema kuanza kupokea vifaa hivyo ni matarajio ya kupokea vifaa vingi zaidi.
Amemshukuru Rais Samia kwa kuwaona na kumuomba kuwapelekea madktari na wataalamu zaidi kwaajili ya kuwapatia huduma.
Kisiwa cha Rukuba kimekamilisha ujenzi wa kituo chake cha afya na tayari kimeanza kupokea vifaa tiba vya kituo hicho.
Akizungumza kisiwani hapo,mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema serikali inawapenda wananchi wake na maombi yao ya kupatiwa wataalamu yatafanyiwa kazi.
Amesema utoaji wa huduma za afya ndani ya jimbo la Musoma Vijijini unaendelea kuboreshwa na kuimarika. Kwa sasa.
Muhongo amesema hospitali ya halmashauri
yenye hadhi ya Wilaya imeanza kutoa huduma na wananchi wameondokana na kusafiri kutafuta huduma za afya.
Amesema ituo vya fya sita (6) vya Murangi, Mugango, Bugwema, Makojo, Kiriba na Kisiwa cha Rukuba vimeanza kutoa huduma.
Ameongeza kuwa zipo zahanati 42; 24 za serikali na 4 za binafsi huku 14 zinajengwa katika lengo la kutoa huduma za afya.
Mbunge huyo amesema wamepeleka maombi serikalini kupata wafanyakazi wa kutoa huduma mbalimbali za afya kwa kuwa wapo wachache sana na kuomba idadi iongezeke pamoja na vifaa tiba.
Amesema wananchi na viongozi wa jimbo la Musoma vijijini wanaishukuru serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwaajili ya shughuli mbalimbali za kijamii.