Na Magrethy Katengu
Kampuni ya Kitanzania ijulikanayo kama Tunzaa Digitali Holdings Limited imesema itahakikisha inaendelea na ubunifu wa kujikita kutatua changamoto.za tabia za kifedha kwa Waafrika kila.siku kwa kutumia teknolojia Mtandao kununu bidhaa kwa kulipa kidogokidogo na kuletewa popote walipo wateja.
Akizungumza leo Jijini Dar es salaam Mkuu.wa Huduma kwa.Wateja Kampuni ya Tunzaa Abdalah Mwesuwa wakati wa Uzinduzi wa Ushirikiano vodacom kupitiawa Mpesa wateja kuanza kutumia Appilikasheni ya Tunzaa ndani ya apilikasheni ya Mpesa ambapo watumiaji watakuwa wanalipia bidhaa kidogo kidogo.
“Tuzaa inapatikana kwa kupakua apilikasheni kupitia simu janja za mkononi au android iOS, pia watumiaji wanaweza kununua bidhaa kwa kutembelea Tuzaa tovuti ya Tuzaa: www.tuzaa.co.tz“
Mkuu wa Huduma, Abdalah Mwesuwa amesema dhumuni la Tuzaa ni kuweza kuimarisha tabia chanya za kifedha kwa waafrika na kuwezesha kununua bidhaa kwa njia ya awamu bila madeni kwa sasa Tuzaa inatoa huduma zake nchini Tanzania nzima na badae kutakua na wigo wa kufikia nchi jirani kama kenya, uganda, kongo, zambia, malawi, na msumbiji.
Kwa sasa wateja wa vodacom wanaotumia huduma ya mpesa kwa ajili ya kufanya miamala yao wataweza kupata huduma ya kununua bidhaa mbalimbali kwa kulipa kidogo kidogo kutoka kwenye apilikasheni hiyo ya Tuzaa inaenda kusaidia watumiaji wa mpesa kuweza kufanya miamala ya kununua bidhaa wakiwa wanaendelea na huduma nyingine za mpesa
Kwa Upande Meneja Malipo ya Kidigital na Channel za Mtandaon Josephine Mushi amesema Ushirikiano wao na M-Pesa ni uthibitisho wa dhamira yetu ya pamoja ya kuwezesha watanzania na Waafrika wa kawaida kupata suluhisho la kupata bidhaa bora kwa njia ya kulipa kidogokidogo
, Faida ya kutumia.kampuni hii kupitia aplikesheni ya Tunzaa kupata bidhaa kwa urahisi , watumiaji wanaweza kufikia jukwaa la “Hiadhi sasa nunua baadaye” la Tunzaa moja kwa moja ya Programu ya M-Pesa bila haja ya kutumia tovuti”amesema Josephine
Aidha Kampuni ya Tunzaa lilibuniwa kwa.lengo.la kuwezesha.Waafrika wa.kawaida.kupata bidhaa kwa.awamu bila deni kwa dhamira ya kuingiza fedha kidogokidogo na inatoa njia salama bora na endelevu kwa watumiaji kupata bidhaa na huduma.wanazohitaji.