Jeshi la zimamoto mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na Wakala wa Vipimo WMA wametoa elimu ya kujilinda moto na jinsi ya kuhakiki ujazo wa gasi kwa wauza mtumiaji wa mitungi ya gasi ya Oryx wa Wilaya ya Kibaha ili kuwalinda na athari za moto na Wananchi wapate gasi yenye ujazo unaowiana na pesa waliyolipa.
Akitoa mada kwenye Kongamano la mwaka la Wafanyabishara wa uzalilishaji wa mitungi ya gasi ya Oryx mjini Kibaha mkoani Pwani Afisa Wakala wa Vipimo WMA mkoa wa Pwani Isaack Bilahi amesema kutoa elimu ya uhakiki ujazo wa mitungi ya gasi kwa wauza wa mitungi ya gasi ni kutimiza takwa la kisheria.
Amesema muuzaji wa mitungi ya gasi ahakiki ujazo wa mitungi ya gasi kwa kupima mmoja mmoja wakati anapokea mzigo kutoka kwa muuzaji wa jumla na hata wakati wa kumuuzia Mteja kabla ya kumkabidhi inabidi ahakikishiwe ujazo na uzito wa mtungi anaouziwa kama unalingana na ujazo na uzito sahihi wa mtungi anaohitaji.
Bilahi amesema wauzaji wa mitungi wahakikishe wanauzia wateja mitungi ya gasi iliyokidhi viwango vya ujazo na uzito wa gasi inayotakiwa na Mteja kulingana na kiasi cha pesa stahiki.
Amesema lengo la serikali kuagiza Wakala wa Vipimo WMA kusimamia upimaji wa mitungi hiyo ya gasi ni kumlinda Mteja apate gasi yenye ujazo na uzito sahihi kulingana na kiasi cha pesa stahiki cha malipo ya gasi anayohitaji.
Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Jeshi la Zimamoto mkoa wa Pwani Surgent Banasani Janja amesema duka la uzalilishaji wa mitungi ya gasi hapatakiwi kuwa na uvutaji sigara karibu hivyo pia katika ukaguzi watakaofanya watahakiki kama dukani hapo Kuna bango la “usivute sigara”
Amesema pia watakagua kwa kuona kama dukani hapo Kuna mitungi ya kuzima moto “fire extinguisher”
Aidha Surgent Janja amewataka wauzaji hao wa mitungi ya gasi kuzingatia kutoa taarifa ya moto mapema wakati moto ukiwa katika hatua zake za mwanzo ili iwe rahisi kudhibiti iwapo moto utatokea badala ya kuchelewa kutoa taarifa jambo ambalo hupelekea athari kubwa za moto kwa wanapatwa na janga Hilo.
Afisa Masoko wa ECO Africa Abdullatif Jafar Abeid amewataka wauzaji hao wa mitungi ya gasi ya Oryx na Watanzania kutumia vifaa vya kuunganisha jiko na mitungi ya gasi vyenye ubora ilkudhibiti matukio ya moto na usalama wao.
Abdul aliitaja baadhi ya vifaa hivyo kuwa ni pamoja na mipira ya gasi, banner, majiko yenyewe na viberiti vyote kutoka ECO Africa ambavyo vina ubora na ni madhubuti.
Naye Afisa masoko wa Kampuni ya Oryx Tanzania Kisaka amesema kuhusu kuunga mkono jitihada za serikali za kulinda na kutunza mazingira kwani tayari Kampuni hiyo imekwishagawa mitungi ya majiko 1800 kutoka serikalini kupitia REA kwa kushirikiana na wabunge wa mkoa huo ambapo pia Kampuni hiyo ya oryx yenyewe iratoa tena mitungi 1800 katika maeneo hayo hayo ya mkoa huo.
Amesema ugawaji huo wa mitungi unaonyesha ni jinsi gani biashara hiyo ya kuuza mitungi ya gasi inakuja kuhimalika zaidi mkoani Pwani tofauti na ilivyosasa.
Kampuni hiyo imejidhatiti kuboresha na kuongeza wigo wa kutoa huduma zake katika kuhudumia Wananchi mkoani humo.