Washindi elfu ishirini na nane mia sita (28,600) wamepatikana kwenye kampeni ya Cha wote kutoka tigo tokea kuanza kwa kampeni hiyo iliyodumu kwa siku tisini
Hayo ameyasema Mary Rutta Meneja wa kitengo Maalum tigo pesa leo Septemba 22, 2023 wakati akikabidhi baadhi ya wawakilishi zawadi ya hundi ya milioni Moja Ofisi za Tigo Jijiji Dar es salaam
Ameongezea kwa kusema watumiaji wa mtandao huo waendelee kuwa karibu na huduma zao kwani kuna mambo kibao yatakayokuja kwa wateja wao
Naye Mshindi Devotha Kweka kutokea Dar es salaam amejishindia milioni moja amesema fedha hizo zitamsaidia kukuza biashara yake na mambo yake binafsi
Kampeni hiyo ikiwa imefikia tamati imedumu kwa siku tisini miongoni mwa zawadi zilizokuwa zinatokewa ni Milioni tano bonasi ya dakika na SMS