Home Afya WITO WATOLEWA KWA JAMII KAGERA KUHAKIKISHA WATOTO CHINI YA MIAKA 8 WANAPATIWA...

WITO WATOLEWA KWA JAMII KAGERA KUHAKIKISHA WATOTO CHINI YA MIAKA 8 WANAPATIWA CHANJO YA MATONE YA POLIO

Na Theophilida Felician Kagera.

Mkuu wa wilaya Bukoba Mkoani Kagera Erasto Sima ametoa wito wakuwahimiza wazazi, walezi na jamii kwa ujumla mkoani Kagera kuhakikisha kila mtoto mwenye umri chini ya wa miaka nane (8) anapatiwa chanjo ya matone ya polio.

Ameyasema hayo hii leo Tarehe 22 Desemba 2023 akiwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe. Fatma Mwassa katika zoezi la uzinduzi wa kampeni hiyo inayoendelea kufanyika kwa sasa Mkoani humo zoezi lililofanyika kituo cha afya Rwamishenye Manispaa ya Bukoba.

Ameeleza kuwa zoezi hilo tayari limeanza tangu Tarehe 21 na litahitimishwa tarehe 24 Desemba mwaka huu, hivyo kila mtoto mwenye umri lengwa anatakiwa kupewa matone hayo kwa ajili ya kumkinga dhidi ya ugonjwa wa polio.

Amefafanua kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekuwa ikifanya kila namna ya kuwakinga watoto ili waweze kubakia salama dhidi ya milipuko ya magonjwa tofauti tofauti ambapo ameyataja baadhi ya mgaonjwa yanayokingwa kwa chanjo hapa nchini ni pamoja na polio, kifua kikuu, surua, donda koo, pepo punda, uvico 19, homa ya ini na mengineyo.

Amesema kwamba ugonjwa wa polio unasababisha madhara makubwa yakiwemo ya ulemavu wakudumu sambamba na kifo hivyo ni muhimu zaidi kwa watoto kupata chanjo hizo ili kuwasaidia kuepuka na madhara hayo.

Ameendelea kueleza kuwa zoezi hilo nila muda wa siku nne kwahiyo jitihada za makusudi zinahitajika ili watoto wote lengwa wapatiwe chanjo kwani nihaki yao ya msingi.

Amewahakikishia wananchi kuwa chanjo ya polio ni imara na salama kwa ajili ya afya ya watoto hivyo ametoa wito akisisitiza kuwa asiwepo mtu wakugomea mtoto kupata chanjo kwaimani potofu kwani kufanya hivyo nikumnyima haki mtoto jambo ambalo halitokubalika.

“Zoezi hili linaweza kuwa linafanyika akawepo mtu wakumficha mtoto wake nyumbani mimi niwambieni sisi kama wazazi sisi kama viongozi tuangalie katika mazingira yetu yapo mambo makubwa yaliyosabaishwa na madhara ya polio kutokana nakutokupata chanjo hizi zamani, sisi tuliopata tuko vizuri hivi lakini wapo wengine tuliozaliwa nao hawapo leo wengine niwalemavu yote hiyo kwa sababu hawakupata chanjo hiyo” amesema Mkuu wa wilaya Erasto Sima.

Baada ya mengi hayo ameishukuru Serikali kupitia wizara ya Afya kwakuendelea kutoa huduma za chanjo kwa watoto Kagera na kwingineko kwa malengo ya kuwakinga na maradhi ya milipuko ya magonjwa ukiwep polio, huku akiwashukuru na wadau mbalimbali ambao wamekuwa bega kwa bega na kuiunga mkono Serikali kwa namna mbalimbali hususani shirika la Afya Duniani WHO pamoja na Shirika la kuhudumia watoto UNICEF ambao pia wameshiriki katika uzinduzi huo.

Aidha amewaagiza viongozi,watendaji wote kwa kila mmoja awajibike kwanafasi yake katika kuhakisha zoezi hilo linafanyika vyema na kwa usahihi ili kufanikiwa kwa kiwango zaidi.

Mratibu wa chanjo mkoa Kagera Zabloni Segeru akitoa taarifa amesema kuwa wanatarajia kuwafikia watoto wapatao (729387) watapatiwa chanjo hiyo ambayo inatolewa mikoa 6 ukiwemo Kagera, Kigoma, Songwe, Mbeya, Katavi na Rukwa.

Ameongeza kuwa tangu siku moja kuanza kwa zoezi hilo linaendelea vizuri maeneo yote ya Mkoa na tayari wemechanja 45% yalengo liliokusudiwa.

Mganga Mkuu wa Mkoa Kagera Issessanda Kaniki amewashukuru wananchi waliojitokeza kituoni hapo wakiwa na watoto kwa ajili ya kupata chanjo ambapo amebainisha kuwa wao kama serikali ya Mkoa kwakushirikiana na wadau wamejipanga vizuri katika kuhakikisha zoezi hilo linatekelezwa nakufanikiwa kwakiwango cha juu.

Baadhi ya wananchi walioshiriki kupata chanjo katika kituo hicho wameishukuru serikali kwa kuleta huduma hiyo yenye kuwasaidia watoto wao dhidi ya ugonjwa wa polio na kutoa wito kwa wazazi wengine kuwapatia chanjo hizo muhimu.

Kauli mbiu ya kampeni hiyo ni kila tone la chanjo ya polio humkinga mtoto dhidi ya ulemavu na kifo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!