Home Kitaifa WATOTO WAIOMBA SERIKALI KUONGEZA NGUVU ZAIDI KATIKA KUKABILIANA NA UVUVI HARAMU

WATOTO WAIOMBA SERIKALI KUONGEZA NGUVU ZAIDI KATIKA KUKABILIANA NA UVUVI HARAMU

Na Theophilida Felician Kagera.

Baadhi ya watoto kata Kemondo Halmashauri ya Bukoba Mkoani Kagera waiomba serikali kuongeza jitihada za kuutokomeza uvuvi haramu ndani ya Ziwa Victoria.

Wameyabainisha hayo kwenye mudahalo wakujadili usawa katika jitihada za kuhimili na kukabiliana na athali za mabadiliko ya tabia ya nchi uliofanyika Kemondo.

Wamesema kwamba kutokana na kuwepo kwa dhana zinazotumika katika shughuli za uvuvi haramu zimekuwa zikiharibu mazalia ya samaki, kuharibu ikolojia ya ziwa Victoria na kupelekea kuwepo kwa mabadiliko ya hali ya hewa maeneo yanayolizinguka ziwa hilo.

Watoto hao wameongeza kuwa kutokana na shughuli za uvuvi haramu kuendelea kufanyika katika ziwa hilo zimepelekea uwepo wa kudorola kwa uchumi wa wananchi kwa ukanda huo ambao wamekuwa wakitegemea pakubwa shughuli za uvuvi.

Hata hivyo wametoa wito kwa serikali wakiiomba kuwashirikisha wadau mbalimbali ili kusaidia kukabiliana na mapambano hayo ya uvuvi haramu ziwa Victoria.

Zainabu Shakiru ni mratibu wa Asasi ya Tumaini women Delopment Association (TUWODEA) amesema kuwa Asasi hiyo imeamua kuwa husisha watoto katika mapambano dhidi ya changamoto ya uvuvi haramu katika ziwa Victoria kwani kundi hilo linaguswa moja kwa moja na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Ametoa wito kwa wavuvi kuacha kutumia zana zisizo rafiki kwa ajili ya kulinda mazalia ya samaki kwamaslahi mapana ya kizazi cha sasa na cha badae.

Charles Charisious mwanasheria ambaye anafanya kazi na taasisi hiyo ya (Tuwodea) ameelezea kuwa kuwepo kwa mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo kwa kiasi kikubwa huchangiwa na shughuli za kibinadamu imeziweka njia panda haki za watoto kwa namna moja au nyingine.

Amefafanua kuwa hali hiyo imesababisha baadhi ya familia kuwa katika hali ngumu kiuchumi hadi kupelekea wengine kutelekeza familia zao kitendo ambacho kinachangia watoto kukosa haki zao za malezo bora.

Amezitaja baadhi ya athali zinazosababishwa na madiliko ya tabia ya nchi ukiwemo uvuvi haramu unaopelekea kupotea mazima kwa aina ya samaki kwani yapo makundi ya samaki hayapendi kelele na vurugu za hapa napale ndani ya maji hivyo hukimbia nakwenda kwenye kina kirefu, migogoro ya kifamilia kutokana na kushuka kwa uchumi wa kifedha na chakula yote hiyo hutokea kutokana na changamoto hizi hususani za uvuvi haramu.

Hata hivyo amehitimisha akitoa wito kwa serikali kuendelea kutoa elimu ipasavyo kwa wavuvi juu ya namna gani waweze kuvua kwanjia zinazokubalika ili kulinda nakutunza samaki na ziwa kwa ujumla huku akiisisitiza jamii nayo kuwajibika katika kutunza ziwa hilo na vyanzo vyamaji vinavyowazunguka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!