Na Shomari Binda-Musoma
JESHI la Polisi mkoani Mara linawashikilia watu 10 wakiwemo walimu 5 kwa kufanya udanganyifu ili wajipatie fedha isivyo halali.
Watu hao walifanya udanganyifu wa nyaraka mbalimbali ili wajipatie fedha kutoka chama cha ushirika cha Chogo Credit Company Limited kilichopo mjini Musoma.
Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Mara Salim Morcase amesema kufanikiwa kukamatwa kwa walimu hao pamoja na watu wengine wa 5 ni ushirikiano kutoka kwa watumishi wa ushirika huo.
Kamanda Salim amewataja walimu waliokamatwa kuwa ni Pashal Gaspel, mwalimu shule ya msingi sabasaba mkoani Mwanza, Meryciana Bhoke wa shule ya msingi Kisesa, Katambi Mganga wa shule ya msingi Giriku’A’ iliyopo Bariadi mkoani Simiyu, Harimq Bakari wa shule ya msigii Rugee iliyopo wilayani Mwanza na Getruda Hoja mwalimu wa shule ya msingi Kisesa iliyopo mkoani Mwanza.
Kamanda Salim amesema walimu wote walighushi nyaraka mbalimbali na kusaini wanafundisha katika shule mkoani Mara.
Watu wengine waliokamatwa kwenye tukio hill ni Samson Elnest, Innocent Ndeaabura, Getruda Kujerwa na James Sebastian wakazi wa Mwanza pamoja an Martin Kandqyoga mkazi wa Songe mqnispaa ya Musoma.
Kamanda Salim amewataka watumishi wa umma kuzingatia taratibu za sheria na kuacha kushiriki matukio ya kiuhalifu.
Amesema kughushi vyeti kwa lengo la kujipatia fedha kinyume cha utaratibu ni uhalifu kama ambavyo ulivyo uhalifu mwingine.
“Siku hizi njia za kupata fedha hasa kwa watumishi wa umma ni eahisi kutoka kwenye taasiei za kifedha sasa kutumia njia zizisofaa ni kutaka kuishia kwenye mikono ya sheria”, amesema kamanda Salim.