Home Michezo COASTAL UNION WALAMBA DUME UDHAMINI KUTOKA ELSEWEDY CABLE

COASTAL UNION WALAMBA DUME UDHAMINI KUTOKA ELSEWEDY CABLE

Na Boniface Gideon, TANGA

Timu ya soka ya Coastal Union ya Jijini Tanga imemewatambulisha wadhamini wao wapya ambao watakuwa wadhamini kwa msimu mmoja wa ligi 2023/204. Wadhamini hao ni kampuni ya utengenezaji wa Vifaa vya Umeme ya Elsewedy Cable ambaye atakuwa mdhamini Mkuu wa Club na K4 Security Ltd watakuwa ni wadhamini wenza hususani kwenye Ulinzi wa Timu na gharama za Vifaa tiba.

Katika udhamini huo thamani ya udhamini haijawekwa wazi na Mamlaka za Club hiyo pamoja na wadhamini wao. Katibu Mkuu wa Coastal Union Omary Ayoub aliwaambia Waandishi wa Habari mapema Jana jioni kuwa udhamini huo ni kwa msimu mmoja huku kukiwa na kipengere cha kuongeza Mkataba hususani endapo timu hiyo itafanikiwa kupata nafasi ya kuwakiliasha nchi kwenye michuano ya kimataifa.

“Kwenye mkataba wetu tunakipengele Cha kuongeza na hii itatokana na mdhamini Mkuu kuridhishwa na matokeo yetu ama namna tutakavyomtangaza” Alisema Ayoub

Ayoub alisema thamani ya udhamini huo itawekwa hadharani hivi karibuni.

Thamani ya udhamini huu itawekwa hadharani hivi karibuni lakini ifahamike tu kuwa mdhamini amebeba majukumu mengi Sana kwenye klabu yetu hivyo sisi tutahakikisha msimu ujao tunapanda ndege kuwakiliasha nchi kwenye michuano ya kimataifa” Alisisitiza Ayoub

Aliwataka Wanachama na Mashabiki wa Timu kujitokeza kwa wingi uwanjani Wakati timu hiyo inapocheza,

“Kilichobakia ninyie mashabiki na wanachama kujitokeza kwa wingi uwanjani Wakati timu yetu inakuwa inacheza na kwakuanza tunaanza na Simba hivyo nawaomba mjitokeze kwa wingi” Alisema Ayoub

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!