Home Kitaifa Mahafali ya 15 Messa yang’ara

Mahafali ya 15 Messa yang’ara

KUWEPO kwa madarasa ya kulea watoto umri wa kuanzia mwaka na nusu ni njia ya kufanya wazazi wajishughulishe na shughuli za maendeleo bila kuathiriwa.

Hayo yamebainishwa leo na wadau wa elimu kwenye mahafali ya 15 kwa shule ya elimu ya awali na msingi Messa iliyopo Jijini Mwanza ambapo wanafunzi 57 wamehitimu darasa la Saba.

Meneja wa Benk ya NBC Mwanza Innocent Mtenge alisema kuwa wanashukuru shule hiyo kwa kutoa malezi na elimu kwa watoto wadogo kwa kuvumilia mahitaji ya wazazi na walezi katika ulipaji wa ada za wanafunzi.

Mtenge alisema benki hiyo imeanzisha huduma za kuwafungulia watoto walio chini ya miaka 18 akaunti ya Chanua ili kuwawezesha kutumia wanapojiunga na shule kwa ajili ya kupata malezi na elimu.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Emmanuel Benedict alisema watoto 57 waliofanya mtihani darasa la saba watapata alama A kwenye masomo yao yote kutokana na maandalizi ya ukaribu yaliyofanywa kwa wanafunzi hao.

Alisema mwaka jana wanafunzi 53 walipata alama A katika masomo yao yote huku Saba wakipata alama B hivyo mwaka huu lazima wavuke ushindi waliopata kipindi hicho.

Meneja wa shule hiyo Magreth Messanga alisema kuwa wanajitahidi kuwafundisha watoto kuanzia elimu ya awali mila na tamaduni za Kitanzania ili kuwafanya watoto kukua wakiwa na uzalendo kwa nchi yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!