Home Michezo MASHABIKI WA YANGA MUSOMA MJINI WAANZA SAFARI KUELEKEA RWANDA

MASHABIKI WA YANGA MUSOMA MJINI WAANZA SAFARI KUELEKEA RWANDA

Na Shomari Binda-Musoma

WANACHAMA na mashabiki wa timu ya Yanga tawi la Musoma mjini wameanza safari mchana wa leo kuelekea Kigari nchini Rwanda kuishangilia timu yao.

Yanga inatafuta nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa iwapo itaitoa timu ya Al Merrick ya Sudan ambayo imechagua kuchezea michezo yake nchini Rwanda.

Jumla ya wanachama na mashabiki 30 wameinza safari hiyo huku wakiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo.

Mwenyekiti wa Yanga tawi la Musoma Ismail Massaro amesema wanakwenda nchini Rwanda na matumaini makubwa ya kurudi na ushindi.

Amesema wanamuamini kocha Gamondi kuwa amekiandaa kikosi cha kwenda na kurudi na matokeo mazuri nchini Rwanda.

Massaro amesema wanachama na mashabiki tawi la Musoma mjini wameamua kwenda nchini Rwanda huku wakiwa na matumaini makubwa.

“Nawashukuru wanachama na mashabiki walioamua kujitoa na kuchangia safari hii ya kuelekea Rwanda”

“Tumepewa baraka zote na viongozi akiwemo mkuu wa mkoa,Said Mtanda kuhusu taratibu zote zikiwemo za kuvuka mpaka na kuingia nchini Rwanda” amesema Massaro.

Baadhi ya mashabiki hao wamesema wanakwenda kuishangilia timu yao kwa nguvu zote hadi kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!