Home Kitaifa Mitungi ya gesi 400 itatolewa kwa Wajasiriamali wilaya ya Ilemela

Mitungi ya gesi 400 itatolewa kwa Wajasiriamali wilaya ya Ilemela

MITUNGI ya gesi 400 itatolewa kwa kina Mama wajasiriamali wa Jimbo la Ilemela na Mbunge wao ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Angelina Mabula kwa ajili ya kupambana na uharibifu wa mazingira.

Hayo yamebainishwa na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Charles David alipokuwa akizungumza na Chombo hiki Cha Habari alisema Lengo la kutoa huduma hiyo kwa kundi hilo ni kuondoa changamoto ya matumizi ya Kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia.

Alisema wamelenga kundi hilo la kina mama kwani ndo wanaoathirika na matumizi ya nishati isiyo rafiki kwa afya na huchangia uharibifu wa mazingira hali inayoendelea kuleta wasiwasi kwa usalama wa wanadamu hapa duniani.

David alisema zoezi la utoaji wa mitungi hiyo ya gesi ya kupikia itafanyika Septemba 16 katika Viwanja vya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!