Home Michezo NYAKATO FC YA KWANZA KUTINGA NUSU FAINALI MASHINDANO YA MATHAYO CUP

NYAKATO FC YA KWANZA KUTINGA NUSU FAINALI MASHINDANO YA MATHAYO CUP

Na Shomari Binda-Musoma

TIMU ya Nyakato fc imekuwa ya kwanza kutinga nusu fainali ya mashindano ya Mathayo Cup kwa kuifunga timu ya Kitaji fc bao 1-0.

Bao pekee la Nyakato fc limefungwa na mchezaji wake Peter Mayemba katika dakika ya 85 ya mchezo huo uliofanyika uwanja wa Mara sekondari.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo,kocha wa timu ya Kitaji fc Zamoyoni Taruma amesema wachezaji wake hawakushika maelekezo yake na kupelekea kupoteza mchezo huo.

Amesema walikuwa na malengo ya kufika mbali zaidi na hata kuchukua ubingwa lakini malengo hayakuweza kufikiwa.

Kwa upande wake meneja wa timu ya Nyakato, Zakayo Zakayo amewapongeza wachezaji wake kwa kucheza mchezo mzuri uliopelekea kushinda na kutinga nusu fainali.

Amesema mchezo huo umemalizika na sasa wanajipanga na mpinzani atakayekuja kwenye hatua ya nusu fainali.

“Mchezo ulikuwa mgumu lakini vijana wamepambana na kutupa ushindi na sasa tunajiandaa na mchezo ujao”

“Tunawaomba wananchi wa Kata ya Nyakato kuendelea kutuunga mkono ili msimu huu ubingwa uelekee nyumbani” amesema Zakayo.

Robo fainali ya pili ya mashindano hayo itapigwa kesho kwenye uwanja huo wa Mara sekondari kati ya timu ya Mwisenge na Nyamatare.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!