Home Kitaifa RC MTANDA AWAALIKA WANANCHI MAONYESHO YA “MARA DAY” WILAYANI SERENGETI

RC MTANDA AWAALIKA WANANCHI MAONYESHO YA “MARA DAY” WILAYANI SERENGETI

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa mkoa wa Mara, Said Mtanda amewaalika wananchi kwenye naadhimisho ya maonyesho ya “Mara Day” yanayoanza kesho wilayani Serengeti.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake amesema maonyesho hayo yana umuhimu mkubwa kwa kuwa yapo mambo ya kujifunza.

Amesema suala hifadhi wa bonde la mto Mara ni moja ya mambo wananchi watakayojifunza kupitia maonyesho hayo.

Mtanda amesema.mwaka huu ni zamu ya mkoa wa Mara kuandaa maonyesho hayo ambapo wageni kutoka ndani na nchi jirani ya Kenya wanatarajiwa kushiriki.

Amesema uzinduzi wa maadhimisho hayo utafanywa na Naibu Waziri wa Maji,Merrypriscal Mahundi September 12 na yatadumu hadi September 15.

Amesema maandalizi yote yamekamilika ya kufanyika kwa maonyesho hayo mwaka huu huku wadau mbalimbali wakiwa wamejitokeza kushiriki.

“Niwaombe wananchi kuanzia septemba 12 hadi 15 pale Serengeti tujitokeze kutembelea maonyesho ya maadhimisho haya”

“Yapo mambo ya kujifunza ikiwa ni pamoja na uhifadhi wa bonde la mto Mara na mazingira yanayozunguka” amesema RC Mtanda.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema katika miaka ijayo maonyesho hayo yatafanywa kuwa makubwa zaidi katika kuutangaza mkoa wa Mara kama ambavyo mikoa mingine inafanya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!