Home Kitaifa DKT. MPANGO AAGIZA MRADI WA MAJI WA MAJIMOTO UKAMILISHWE HARAKA

DKT. MPANGO AAGIZA MRADI WA MAJI WA MAJIMOTO UKAMILISHWE HARAKA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameitaka Wizara ya Maji kusimamia mradi wa maji wa Majimoto ulioko Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani Katavi ukamilike haraka.

Mhe. Mpango amesema hayo Julai 22 wakati wa hafla fupi ya Uzinduzi wa jengo la utawala la halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe.

Amesema mradi huo unaumuhuhimu mkubwa kwa wananchi wa Mpimbwe hivyo ni vema ukakamilika kwa haraka ili wananchi waondokane na changamoto ya upatikanaji wa majisafi, salama na yenye kutosheleza.

Vilevile ameitaka Wizara ya Maji ijipange ili ianze kutumia chanzo cha uhakika cha maji kutoka ziwa Tanganyika kwa ajili ya kuhudumia mkoa wa Katavi.

Anzeni kujipanga kuanza kutumia maji ya uhakika ya ziwa Tanganyika kwa ajili ya kuhudumia mkoa wa Katavi. Najua ni mradi mkubwa na utatumia gharama kubwa, lakini inawezekana kama ambavyo imewezekana kuyasafirisha maji ya ziwa Victoria hadi Tabora.” Mhe. Mpango amesema.

Awali akiongea katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amesema Wizara ya Maji inaendelea na mipango ya kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wananchi wote wa mkoa wa Katavi.

Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameelekeza kiasi cha shilingi bilioni 3.4 kwa ajili ya upanuzi wa mradi wa maji wa Majimoto hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi. Pia wizara inanaendelea na utekelezaji wa miradi mingine ili kuhakikisha wananchi wa Mpimbwe wanapata maji ya kutosha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!