Home Biashara MBAGALA YAZIZIMA TIGO WAKITOA MILIONI 5 KWA MSHINDI WA CHA WOTE

MBAGALA YAZIZIMA TIGO WAKITOA MILIONI 5 KWA MSHINDI WA CHA WOTE

 Na Mwandishi Wetu.

 Bi Halima Rajabu Seleman Mfanya biashara ndogondogo mkazi wa Kilungule – Mbagala Jijini Dar Es Salaam ni miongoni mwa washindi wa Milioni TANO Kampeni ya Tigo CHA WOTE ambapo hadi sasa imebaki wiki moja tu Kutamatisha Kampeni hii iliyowanufaisha wateja wengi Tigo wameshatoa Fedha Taslim na zawadi mbalimbali kwa Washindi zaidi ya elfu 24 Nchi Nzima 

Akizungumza Leo Septemba 8, 2023. Wakati wa Kumkabidhi Mshindi Bi Halima Mfano wa Hundi ya Milioni Tano maeneo ya Mbagala Zakiem Jijini Dar Es Salaam , Meneja Wa Kanda Bwn.  Jansen Msechu amesema kuwa hadi sasa ikiwa imebaki Wiki moja kampeni Ya Cha Wote iishe wameshapatikana washindi zaidi ya elfu 24 kutoka maeneo mbalimbali nchini .

” Leo tunayo furaha kubwa kumkabidhi Bi Halima Milioni Tano yake , Lakini niwakumbushe Watanzania kwamba kila siku CHA WOTE inatoa zawadi ikiwemo pesa taslimu hadi Milioni Moja kwa washindi 320 kila siku , Pamoja Na zawadi za dakika na SMS kwa watumiaji wa Mtandao wa Tigo, kuibuka mshindi ni rahisi tu unachotakiwa ni kufanya miamala na Tigo Pesa kama Kutumia Lipa Kwa Simu , Kununua Vifurushi , Kulipia Bili kwa Tigo Pesa , n.k kwa kufanya ivyo nawewe siku si nyingi utakua miongoni mwa Washindi wa Kampeni hii ya CHA WOTE ndani ya hii Wiki iliyobakia “. amesema Bwn Jensen

Naye kwa Upande Wake Bi Halima mmoja wa washindi WA Milioni Tano , ameipongeza sana Kampuni ya Tigo kwa zawadi hii na kusema kuwa Milioni TANO hii itamsaidia sana kuboresha biashara zake ndogondogo anazozifanya 

” Kwakweli asanteni sana Tigo na nawasihi watanzania wafanye miamala kwa wingi,  kununua vifurushi na Lipa kwa Simu maana ndo siri pekee ya Ushindi ” Alimalizia Bi. Halima

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!