Home Kitaifa BAADHI YA BODABODA MJINI MUSOMA WATOA TAMKO LA KUTOSUSIA KUNUNUA MAFUTA

BAADHI YA BODABODA MJINI MUSOMA WATOA TAMKO LA KUTOSUSIA KUNUNUA MAFUTA

Baadhi ya viongozi wa Bodaboda Musoma mjini wamesema hawajawahi kutoa tamko la kususia kununua mafuta ktk kituo cha The White Co (LTD) kama ilivyotangazwa na baadhi ya vyombo vya habari hivi karibuni kufuatia boda boda mmoja kuuawa wakati akijaribu kumshambulia mlinzi wa kituo hicho.

Msimamo huo wameutoa leo na kusema kamwe hawawezi kuunga mkono mawazo ya kikundi hicho kinachotumiwa na chama kimoja cha upinzani kwa malengo binafsi ktk kuleta taaruki na kuvunja sheria za nchi.

Wamesema baada tukio hilo tayari polisi imechukua hatua ya kuchunguza tukio hilo pia kumshikilia mlinzi huyo hivyo hawawezi kuhusisha tukio hilo na biashara hiyo huku wakionya wenzao wanaohujihusisha na uhalifu kisha kujificha kwenye kivuli cha boda boda huku wakijua wanatumiwa kisiasa kwa malengo machafu.

Hata hivyo hivyo wameomba baadhi ya vyombo vya habari kuacha kutumika kwa mgongo wa bodaboda wanaotumiwa kwa malengo yao na kwamba wao hawezi kugomea biashara ya mtu kwa makosa ya mwenzao mmoja.

Wiki iliyopita bodaboda moja alifika kituo hicho usiku na kupewa huduma kisha kuanza kurushiana maneno na mhudumu wa kituo hicho ndipo mlinzi huyo alifika kwa lengo la kutuliza vurugu hizo boda boda huyo alimkaba na kumchania nguo mlinzi huyo ndipo risasi ilipofyatuka na kupiga na kusababisha kifo chake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!