Home Afya MADAKTARI BINGWA TOKA BUGANDO WAENDELEA KUTOA HUDUMA HOSPITALI YA MWALIMU NYERERE MUSOMA

MADAKTARI BINGWA TOKA BUGANDO WAENDELEA KUTOA HUDUMA HOSPITALI YA MWALIMU NYERERE MUSOMA

Na Shomari Binda-Musoma

MADAKTARI bingwa kutoka hospital ya kanda Bugando wameendelea kutoa huduma za matibabu ya kibingwa kwenye hospital ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Matibabu yanayotolewa na madaktari hao ni ya ngozi, magonjwa ya ndani, sikio, koo pamoja na pua.

Mganga mfawidhi wa hospital hiyo, Osmund Dyagura amesema madaktari wameendelea kuwaona wagonjwa kwenye zoezi hilo lililoanza septemba 4 hadi 8 hospitalini hapo.

Amesema hii ni fursa nzuri kuitumia ya kambi ya madaktari hao ambapo wagonjwa kwenye bima na wasio na bima wanapata nafasi ya kutibiwa.

Dyagura amesema kwa wagonjwa wasio na bima wanatibiwa kwa gharama za kawaida za hospital na kuwaomba wananchi kutumia muda uliobaki kufika kupata matibabu.

“Timu ya madaktari kutoka hospital ya kanda Bugando kwa kushirikiana na madaktari wa hapa kwetu wanaendelea kutoa huduma kwa wananchi”

“Huduma za madaktari hawa zitaendelea hadi septemba 8 niwaombe wananchi wenye matatizo wafike ili waweze kuhudumiwa na kurudi kwenye afya njema” amesema Dyagura.

Baadhi ya wananchi waliofika hospitalini hapo kupata matibabu wameushukuru uongozi wa hospital ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kuwaletea huduma ya madaktari bingwa mara kwa mara.

Wamesema kusafiri kufuata huduma ya madaktari bingwa Bugando ni gharama na wanapokuwa wanafika Musoma inawasaidia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!