Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene pamoja na Kamati Tendaji ya maandalizi ya Maadhimisho Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa wametembelea na kukagua maandalizi ya kuelea Siku hiyo.
Maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufanyika Kitaifa Jijini Dodoma katika la Uwanja wa Mnara wa Mashujaa tarehe 25 Julai, 2022 ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.