Na Magreth Mbinga
Waziri wa kazi,vijana na walemavu Mh Joyce Ndalichako leo Julai 22 amekutana na wastaafu ili kusikiliza kero zao ambazo wanakumbana nazo wakati wa kufatilia mafao.
Zoezi hilo limefanyika katika ukimbi wa NSSF Ilala Jijini Dar es Salaam na kusema kuwa kama mtu ana changamoto za mafao kwa NSSF na PSSF apate fursa ya kuelezea changamoto zake.
“Lengo la kufanya hivo nikutokana na uzoefu niliouona ndani ya miezi sita tangu nimeanza kuwa katika ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu nimekuwa nikipata changamoto mbalimbali za wastaafu” amesema Mh Ndalichako.
Aidha Mh Ndalichako amesema zipo changamoto za aina tofauti kuna zile zinazotokana na mapunjo ambapo mafao ya mtu yamehesabiwa tofauti na mshahara wake inasababisha mafao yake kuwa madogo kuliko inavyotakiwa na pensheni yake ya mwezi inakuwa ndogo.
“Kwa muda ambao nimeangalia Dodoma na kwa hapa leo nimeshapata watua ambao kesi yake ipo wazi anachotakiwa kurekebishiwa alipwe pensheni kwa kuzingatia mshahara wake wa mwisho na alipwe haki zake zote alizokuwa anapunjwa”amesema Mh Ndalichako.
Pia Mstaafu aliywjitambulisha kwa jina la Chuki Saidi Kashaija amesema amefanya kazi na Wizara ya Afya toka mwaka 1973 na kustaafu 2014 mpaka kufikia leo Julai 22 hajapata kiinua mgongo chake .
“Toka mwaka 2014 nazungushwa naambiwa niende Dodoma nikifika ninaambiwa nirudi Dar es Salaam nimefika mpaka leo hii nimekuja kuonana na Mh Waziri ili niweze kusaidiwa kupata stahiki zangu”amesema Chuki.
Sanjari na hayo Katibu wa wazee pia mstaafu Kassim Salehe amesema watu wanapo staafu wanategemea wapate pesa zao kwa wakati ili waishi vizuri lakini wamekuwa na maisha magumu kuliko walivyotarajia.
“Wastaafu wanasema kuna nyongeza ya pensheni lakini hatujui kama ipo tunacheleweshewa vipi maana wengine tuna familia zinatuangali tunajiongezea tena maisha mengine “amesema Kassim.