Home Kitaifa WATUMIAJI MAFUTA YA ALIZETI KUTOKA NYIHITA SUNFLOWER WASIFU UBORA WAKE

WATUMIAJI MAFUTA YA ALIZETI KUTOKA NYIHITA SUNFLOWER WASIFU UBORA WAKE

Na Shomari Binda-Musoma

WATUMIAJI wa mafuta ya alizeti yanayozalishwa kwenye kampuni ya Nyihita Sunflower Cooking Oil Production,wamesifu ubora wa mafuta hayo.

Wakizungumza kwenye banda la kampuni hiyo kwenye maonyesho ya biashara ya “Twende Mara” yanayofanyika uwanja wa Mukendo mjini Musoma,wamesema wazalishaji wanaandaa vizuri mafuta hayo na kuwa na ladha nzuri.

Wamesema unapotumia mafuta hayo kwenye chakula hayana halufu mbaya bali yana ladha nzuri na kumvutia mlaji.

Mmoja wa wananchi aliyetembelea banda hilo aliyejitambulisha kwa jina la Samson Chacha,amesema tangu kuyafahamu mafuta hayo na kuanza kuyatumia hajapata malalamiko kwenye familia.

Amesema ni muda amekuwa akinunua mafuta hayo na kuyatumia nyumbani na yameonekana kupendwa kutokana na ladha yake.

Chacha amepongeza wazalishaji wa mafuta hayo kwenye kiwanda kilichopo wilayani Rorya kwa kuwafikishia sokoni mafuta yenye ubora.

“Tunashukuru mkoa wa Mara tunacho kiwanda kinacho tuzalishia mafuta ya kula yenye ubora na ladha nzuri kwenye chakula”

“Tunawaomba kuendelea kuzalisha kwenye ubora huu isije ikatokea baadae uzalishaji na ubora ukawa kwenye hali ya chini” amesema Chacha.

Akizungumza na Waandishi wa Habari waliotembelea kiwanda hicho hivi karibuni, Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Paul Nyihita alisema wamejipanga kufanya uzalishaji wenye ubora wakati wote ili kufanya vizuri sokoni.

Alisema watumiaji wataendelea kupokea mafuta yenye ubora kwa kuwa wamedhamilia kuwahudumia vizuri zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!