Viongozi mbalimbali wakipiga makofi kufurahia uzinduzi wa jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika lililozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan jijini Arusha. Jengo hilo limejengwa kwa ubia wa Serikali kupitia TCRA na PAPU kwa uwiano wa 60:40. Anayeonekana akifunua pazia kwenye jiwe la Msingi pamoja na Mhe. Rais ni Mtendaji Mkuu wa PAPU Bw. Chifundo Moyo. Picha: Hisani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt Jabiri Bakari, muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi kama ishara ya uzinduzi wa jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU), lililojengwa kwa ushirikiano wa Tanzania kupitia TCRA na PAPU eneo la Sekei, Arusha. Uzinduzi ulifanyika Jumamosi Septemba 2, 2023.
Sehemu ya washiriki wa hafla ya uzinduzi wa jengo la makao makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU) wakifuatilia kwa makini matukio ya uzinduzi. Jengo hilo limejengwa na kukamilika katika eneo la Sekei, Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali na Umoja wa Posta Afrika (PAPU), muda mfupi baada ya kukamilisha uwekaji wa jiwe la msingi kuzindua jengo la makao makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU) lililopo eneo la Sekei, Arusha. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Selemani Kakoso (Mb), Mhe. Dkt. Khalid S. Mohamed – Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano, na Uchukuzi (SMZ), Mhe. Nape Moses Nnauye – Waziri wa Habari, Mawasiliano, na Teknolojia ya Habari (WHMTH), JMT, Bw. Sifundo Chief Moyo – Mtendaji Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU), Dkt. Beaula Chirume – Katibu Mkuu Wizara ya Tehama, Posta, na Huduma za Vifurushi ya Jamhuri ya Zimbabwe, na Bw. Mohammed Khamis Abdulla – Katibu Mkuu WHMTH.