Na Shomari Binda-Musoma
MFANYABIASHARA mtanzania mwenye makazi nchini Kenya, Ramadhan Msomi ameamua kuwekeza zaidi hapa nchini baada ya serikali kupunguza vikwazo vya uwekezaji.
Uwekezaji alioamua kuwekeza mfanyabiashara huyo ni kwenye upande wa hotel za kifahari, huduma za usafiri wa kitalii nchi kavu pamoja na majini.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Mzawa Blog,Rama amesema kupungua kwa vikwanzo ikiwemo ufatiliaji wa vibali maeneo tofauti umemvutia.
Amesema serikali ya Tanzania imefanya jambo la maana kuvutia wawekezaji wakiwemo wa ndani na nje ya nchini kuja kuwekeza na kuinua uchumi wa nchi.
Rama ambaye amewekeza nchi jirani ya Kenya pamoja na hapa nchini katika sekta ya hotel amesema mwanzo kulikuwa na mambo mengi lakini kwa sasa mambo yako sawa.
Amesema vikwazo ikiwemo mizunguko ya upatikanaji wa vibali imekuwa ikiwafanya wafanyabiashara wengi kushindwa kuwekeza hapa nchini.
“Tumesikia kuwepo kwa dilisha moja la ufatiliaji wa vibali na hii itatusaidia kuja nyumbani kufanya uwekezaji zaidi”
“Nilishaanza kuwekeza hapa nyumbani na kwa utaratibu mzuri uliofanywa na serikali wengi watakuja kuwekezaji zaidi hapa nchini” amesema Rama.
Mfanyabiashara huyo amesema Musoma kwa kuwa ni mahali alipozaliwa ataendelea kufanya uwekezaji zaidi wa huduma za hotel na usafirishaji wa wageni.
Amesema licha ya kuongeza huduma ya hotel kutokana na kuongezeka kwa wageni ameamua kuongeza gari zaidi za utalii na utalii wa majini kwa kutumia boti za “fiber”.