Home Kitaifa WAKUU WA MIKOA WANOLEWA KUTUMIA MATOKEO YA SENSA KATIKA. UTEKELAZAJI WA MAJUKUMU...

WAKUU WA MIKOA WANOLEWA KUTUMIA MATOKEO YA SENSA KATIKA. UTEKELAZAJI WA MAJUKUMU YAO

Na Magrethy Katengu

Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa wametakiwa kutumia matokeo ya sensa kwa wananchi ya mwaka 2022 ili iwasaidie katika kupanga shughuli za kijamii na kiuchumi kulingana na idadi ya watu walionao ili kuleta maendeleo katika mikoa yao kwa usawa

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati katika mafunzo ya usambazaji na matumizi ya matokeo ya sensa kwa wakuu hao wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kamisaa wa Sensa Anna Makinda amesema viongozi hao wanapaswa kutumia matokeo ya sensa katika kupanga shughuli za kimaendeleo katika mikoa yao pamoja na kutoa elimu ya sensa kwa wananchi

Kamisaa wa Sensa Anna Makinda amesisitiza kuwa kuhesabu watu siyo mwisho, kazi kubwa iliyopo mbèle yao na viongozi hao ni kupeleka elimu ya matokeo hayo ya sensa kwa wananchi ili waweze kuyaelewa na kuyatumia katika mipango yao ya maendeleo kwenye maeneo yao husika ya kazi wakati wanaposambaza huduma za kijamii

Sisi wenyewe hatuwezi kumaliza nchi nzima kuanzia ngazi ya Wilaya kata hadi tarafa kwani kutoa elimu hii ya matokeo ya sensa, tunawategemea viongozi hawa na kamati zao za sensa kuyachukua haya na kuyapeleka kwa wananchi, bahati nzuri katika takwimu zetu zipo za hesabu ” alisema Makinda

Hata hivyo ameshukuru pia bidii, ubunifu na kujituma kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala kumefanya zoezi hilo la sensa kuendeshwa kwa urahisi na kufanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu kwani kila mmoja alihusika kwa namna yake licha ya changamoto chache zilizojitokeza lakini kazi kubwa ilifanyika kwa ukamilifu

Naye Mkurugenzi Mkuu wa takwimu NBS Dkt. Albina Chuwa amesema wanawashukuru wakuu wa mikoa kwa kutekeleza na kutoa ushirikiano katika kukamilisha zoezi sensa ya watu na makazi lililofanyika Oktoba 2022 mwaka jana.

Hata hivyo Dk. Chuwa amesema matokeo ya sensa hiyo yameonesha kuwa umri wa mtanzania kuishi umeongezeka kutoka miaka 44 hadi 65 na kwamba hizo ni juhudi ambazo zinafanywa na wakuu hao wa mikoa katika kumsaidia Rais kwenye utendaji kazi wake.

Awali akizungumza kwa Mwenyekiti wa , Mkuu wa Mkoa kutoka Lindi, Zainab Tilak ameshukuru kwa kupatiwa mafunzo hayo na kuwapatia ramani za Sensa zinazoonyesha idadi ya watu walionao katika Maeneo ya kazi kwani ni kutumia matokeo hayo ya sensa ya mwaka 2022 katika kupanga, kupima na kutahimini shughuli za kijamii na utekelezaji wa maendeleo.

Lakini pia yataongeza uelewa wa kutosha wa matumizi wa matokeo ya sensa, sisi kama viongozi wa mikoa matokeo haya yatatusaidia katika kufanya maamuzi ya kitakwimu yanayoakisi hali halisi ya mahitaji ya wananchi,” amesema Zainabu

“Kama tunavyofahamu suala la kupanga maendeleo ni shirikishi na linaanzia kwa wakuu wa mikoa ,Wilaya, Kata,vitongoji na vijiji hivyo kupitia mafunzo hayo watakwenda kuwashirikisha na viongozi wenzao ambao hajahudhuria kuwapatia elimu na ujuzi uzoefu katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku,” amesema Zainabu

Aidha Mwishoni mwa Mafunzo wote waliohudhuria katika Mafunzo hayo walipatiwa ramani itakayowaonyesha namna ya kutumia takwimu kutoa huduma za kijamii kulingana na idadi ya watu wa maeneo husika

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!