Home Kitaifa TPA yaibuka kidedea Maonesho ya Biashara

TPA yaibuka kidedea Maonesho ya Biashara

Na Neema Kandoro, Mwanza

MAMLAKA ya Bandari Tanzania (TPA) imeibuka kidedea kwenye maonesho ya biashara kwa nchi za Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza kutokana na maboresho ambayo yamefanywa kwa zaidi sh bilioni 500 zilizotolewa mwaka jana na serikali.

Meneja Uhusiano na Mawasiliano TPA Nicodemus Mushi alisema serikali ya awamu ya sita imeboresha mazingira ya ufanyaji kazi kwenye bandari ndani ya bahari na maziwa kwenye sehemu zote hapa nchini na hivyo kuwaomba watumiaji wa bandari watoe ushirikiano wa haraka kwa taasisi wanazoshirikiana nazo ili kuwezesha upakuaji wa haraka kwa mizigo yao.

“Tumeboresha vilevile suala la usalama wa mizigo inayopitia kwenye bandari zetu kutokana na uimara wa ulinzi na usalama unaopatikana kwenye bandari zetu hivyo kukidhi viwango vya kimataifa” alisema Mushi

Alisema fedha hizo zimesaidia kuboresha mifumo ya teknolojia ya upakuaji wa mizigo kwa haraka kwenye bandari mbalimbali hapa nchini hivyo kuondoa ucheleweshaji wa kupakia na kupakua mizigo inayoletwa na kusafirishwa.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe alisema kuwa maonesho hayo ya 18 kwa Afrika Mashariki ni fursa kwa wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa kubadilishana uzoefu na maarifa kwa ajili ya kuboresha huduma zao.

Aliwaomba watanzania kutumia nafasi nafasi ya kijiografia pamoja na utulivu uliopo hapa nchini kwa ajili ya kuwekeza katika sekta za uzalishaji mali kwani Tanzania ni nchi ambayo iko katika katika mataifa ya Ukanda wa Afrika Mashariki.

Kigahe aliziomba sekta binafsi na umma kuweka juhudi kubwa katika kuboresha shughuli zao kutokana na serikali kuanza kuweka teknolojia za kisasa katika bandari zote ili kuwepo na ufanisi mkubwa kwa utendaji kazi.

Maonesho ya 18 ya biashara Afrika Mashariki yenye kaulimbiu ‘Mazingira bora ya biashara ni kivutio cha kukuza uwekezaji wa biashara, viwanda, na kilimo Afrika Mashariki’ yanahusisha bidhaa za uhandisi, ujenzi, kilimo, ufugaji, vifungashio, Ngozi, nguo, usindikaji chakula, vinywaji, Sanaa za mikono, vipodozi, urembo, madini, taasisi za fedha, afya na dawa asilia, na mafunzo na ushauri.

Naye Afisa Habari wa Wakala wa Usajili Biashara na Leseni (Brela), Gloria Mbilimonywa, amesema “kutokana na ukuaji wa biashara na viwanda katika Jiji la Mwanza kupitia maonesho haya wanatoa huduma za papo kwa hapo za usajili wa biashara, leseni, viwanda na alama za biashara,

Aliongeza kusema kuwa pia wanaendelea kuboresha huduma zao ziwe rafiki na gharama nafuu kwa kuwepo na usajili wa makampuni kwa njia y a mtandao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!