Home Kitaifa Polisi Mguu sawa maonesho ya Afrika Mashariki

Polisi Mguu sawa maonesho ya Afrika Mashariki

Maonesho ya 18 ya Afrika Mashariki yameanza kufanyika Jijini Mwanza kuanzia Agosti 25, 2023, na kufikia tamati Septemba 3, mwaka huu kwa wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya kuonyesha bidhaa zao.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza nalo mbali na kuweka mikakati ya kiusalama katika maonesho hayo pia tayari limeweka banda la Polisi kwa ajili ya kutoa elimu ya masuala mbalimbali ya kiusalama kwa wananchi watakao tembelea viunga vya furahisha wilaya ya Ilemela yanapofanyika maonesho hayo kwa ajili ya kujifunza.

Maonyesho ya mwaka huu yatazinduliwa na Waziri wa Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji ambapo pia yatashirikisha zaidi ya wafanyabiashara 400 kutoka ndani na nje ya Ukanda wa Afrika Mashariki chini ya uratibu wa Chemba ya Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Mkoa wa Mwanza.

Miongoni mwa faida za kushiriki maonesho hayo ambayo kiingilio chake ni bure kwa wananchi, wafanyabiashara wataonesha na kuuza bidhaa na kutoa huduma za kujifunza, kubadilishana ujuzi na uzoefu pia kuingia mikataba ya uwekezaji na biashara.

Toka Dawati la Habari Polisi Mwanza

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!