Home Michezo IVO MAPUNDA AWATENGENEZA MAKIPA BIASHARA UNITED KUWA TISHIO

IVO MAPUNDA AWATENGENEZA MAKIPA BIASHARA UNITED KUWA TISHIO

Na Shomari Binda-Musoma

KOCHA wa makipa wa timu ya Biashara United inayojiandaa na ligi ya Champion Ship,Ivo Mapunda,amesema anawaandaa makipa wa timu hiyo kuwa tishio langoni.

Akizungumza na Mzawa Blog kwenye mazoezi ya timu hiyo,amesema.golikipa kwenye timu ni sehemu ya ulinzi hivyo anawaandaa kuwa walinzi imara.

Amesema tangu amejiunga na timu ya Biashara United ameendelea kuwajengea uwezo wa makipa wake kujiamini wakiwa langoni.

Ivo amesema makipa alio nao kikosini ni wazuri na namna anavyowaandaa anaamini watakuwa tishio kwenye ligi ya Championi Ship.

Kocha huyo ambaye alipata kuichezea timu ya Yanga kwa mafanikio amedai maumbo ya waliyonayo makipa waliopo kwenye kikosi na kushirikiana na safu nzima ya ulinzi hawataruhusu magoli ya kizembe.

“Tupo na makipa wazuri ndani ya kikosi na namna nnavyowajenga kulitumia lango vizuri watakuwa tishio kwenye ligi ya Champion Ship msimu huu.”

“Najua mashabiki wa Biashara United na wadau wa soka wanatamani kurejea ligi kuu nami kwa kushirikiana na makocha wenzangu tutapambania hill” ,amesema Ivo.

Amesema.kikubwa ni kuwa na ushirikiano na panda zote ikiwemo mashabiki na wadau ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Timu ya Biashara United ipo kwenye mazoezi makali ikiwa ni maandalizi ya ushiriki wa ligi ya Champion Ship katika kampeni ya kurejea ligi kuu msimu ujao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!