Home Kitaifa Wamiliki wa Magari yasiyo na bima waonywa

Wamiliki wa Magari yasiyo na bima waonywa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Wilbrod Mutafungwa amewaonya wamiliki wa vyombo vya moto wanoruhusu vyombo vyao kuingia barabarani huku vikiwa havijakatiwa bima.

Onyo hilo limetolewa leo Agosti 24, 2023 na Kamanda Mutafungwa wakati wa kikao na waendeshaji wa vyombo vya moto na viongozi wao, RATRA, TARULA, TANROAD, AFISA MIPANGO MIJI pamoja na wadau wengine wa usalama barabarani wa jijini Mwanza.

Kamanda Mutafungwa amesema baadhi ya wamiliki wa vyombo vya moto wamekuwa hawakati bima kwenye vyombo vyao hali inayosababisha usumbufu kwa madereva wao hususan zinapotokea ajali.

“Nakuagiza RTO na timu yako tengeneza utaratibu wa kukagua bima kwenye magari na vyombo vingine na ikibainika chombo chochote kinachotakiwa kuwa na bima na hakijakatiwa bima mmiliki apelekwe mahakamani” amesisitiza Mutafungwa

Aidha, amemtaka Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa Mrakibu msaidizi wa Polisi (ASP) Sunday Ibrahim kuchukua hatua kali na za kisheria kwa madereva wote wanaokatisha njia nyakati za jioni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!