Home Kitaifa NYIHITA, RAMA MSOMI WACHANGIA SHULE YA MSINGI KINESI “B” NA KUTOA NENO...

NYIHITA, RAMA MSOMI WACHANGIA SHULE YA MSINGI KINESI “B” NA KUTOA NENO KWA WANAFUNZI

Na Shomari Binda-Rorya

MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi (CCM) Mkoa wa Mara, Nyihita Paul na mfanyabiashara, Rama Msomi wamechangia fedha na vifaa vya michezo kwenye shule ya msingi Kinesi “B”.

Akizungumza kwenye mahafali ya shule hiyo mara baada ya kuchangia kiasi cha shilingi milioni 1 na laki 1,jezi seti 4 na mipira 4 kwa timu ya mpira wa miguu na pete,Rama amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili kupata faida ya elimu.

Amesema elimu ndio suala la msingi kuliko kitu chochote kwa kuwa asilimia kubwa ya waliofanikiwa ni wale waliozingatia elimu.

Rama ambaye ni mfanhaboashara aliyewekeza ndani na nje ya nchi,amewaeleza wanafunzi hao wanaohitimu elimu ya msingi hususani watoto wa kike kukataa kulubuniwa na mambo yasiyofaa bali wazingatie elimu.

Shule hii ya Kinesi B ndio nilikupatia elimu yangu ya msingi na licha ya kuwachangia kama mlivyoomba kwenye risala yenu nawaomba msome kwa bidii”

“Elimu ndio msingi wa maisha nawakumbusha pia Wazazi mliohudhulia mahafali haya tusikimbilie kuwaozesha watoto wetu wa kike bali tuwape elimu”, amesema Rama.

Kwa upande wake Nyihita ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Nuihita Sunflower oil production aliyewakilishwa na meneja wa kampuni hiyo,Happness Masunga,amewakumbusha wanafunzi hao umuhimu wa elimu.

Amesema mkurugenzi Nyihita kama mzazi anapenda elimu na amemuagiza kusisitiza wanafunzi kuzingatia masomo na kuwasikiliza walimu wakiwa darasani.

Amesema Nyihita kama.mzazi amewachangia shilingi laki 6 kwenye ununuzi wa mashine ya kudurufu karasi “photocopy” na kuahidi kuendelea kuchangia kila arakapopata nafasi.

Kwa upande wao walimu na wanafunzi wa shule hiyo wamewashukuru wachangiaji hao na kuahidi kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!