Rais wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Musevani leo tarehe 21 Julai 2022 amewasili nchini Tanzania na kupokelewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda (Mb) katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Mhe Museveni amewasili nchini kwa ajili ya kushiriki kwenye Mkutano wa 22 wa Wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika kuanzia leo tarehe 21-22 Julai 2022 katika ukumbi Ukumbi wa kimataifa wa mikutano-AICC Jijini Arusha.