Home Kitaifa KINANA: UHURU WA KUSEMA UPO ILA KILA UHURU UNA MIPAKA YAKE.

KINANA: UHURU WA KUSEMA UPO ILA KILA UHURU UNA MIPAKA YAKE.

Akumbusha darasa la Hayati Mwalimu Nyerere kuhusu uhuru bila ya nidhamu

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amesema ingawa inchi ina uhuru mkubwa wa kusema na kutoa maoni, lakini ni vyema ukazingatia mipaka.

Kinana ameyasema hayo leo Agosti 22, 2-23 jijini Dar es Salaam wakati katika mkutano wa kitaifa wa wadau kujadili hali ya demokrasia nchini kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).

“Mimi nadhani uhuru wa kusema upo lakini kila uhuru una mipaka yake, Baba wa Taifa (Mwalimu Nyerere) alikuwa akitufundisha kwamba uhuru bila ya nidhamu ni wendawazimu na nidhamu bila ya uhuru ni utumwa, kwa hiyo kila uhuru lazima uwe na mipaka yake lakini nadhani kwa ujumla uhuru upo wa kutosha wakati mwingine labda kuna kasoro katika utekelezaji wake nadhani ndio maana Watanzania wanapiga kelele katika kusimamia sheria zinazowapa Watanzania uhuru wa kusema.” Amesema Kinana

===

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!