Home Kitaifa MGANGA MKUU KAGERA APONGEZA JUHUDI ZA UTEKELEZAJI WA MPANGO JUMUISHI KWA WATOTO

MGANGA MKUU KAGERA APONGEZA JUHUDI ZA UTEKELEZAJI WA MPANGO JUMUISHI KWA WATOTO

Na Theophilida Felician, Kagera

Mganga Mkuu wa Mkoa Kagera Issessanda Kaniki amewapongeza na kuwashukurua wadau mbalimbali kwanamna wanavyoendelea kutekeleza mpango jumuishi wa malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto Mkoani Kagera mpango ambao unatekelezwa nchini.

Kaniki ametoa pongezi hizo kwenye kikao kilichowakutanisha wadau tofauti tofauti kutoka mashirika ya siyo yakiserikali watalaamu kutoka serikalini ambapo maafisa mandeleo ya jamii, maafisa ustawi wajamii kutoka Halmashauri zote za Kagera, waandishi wahabari pamoja na viongozi wa dini.

Awali ameeleza kuwa anashukuru mchango wa wadau wa mashirika ya siyoyakiserikali kwanamna ambavyo yamekuwa yakipambana kwakila namna katika kupiga vita changamoto zinazo wakabili watoto katika jamii ikiwemo hiyo ya utekelezaji wa mpango huo muhimu ambao umeandaliwa na Serikali.

“Moja kwanza niwashuru sana wadau wetu wote wakiwemo TADEPA nawengine wengi bila kusahau waandishi wa habari na vyombo vyahabari kwa ujumla kwakuendelea kuwa bega kwa bega nasisi nashukuru kwa Mkoa Kagera tuna ushirikiano na sehemu zote kwa minajili kwamba watoto wetu wanahitaji kuendelezwa kwa anga zote zinazostahili zaidi na zaidi sekta ya habari ni sekta tunayoitegemea sana katika utekelezaji wa mpango huu na mipango mingine wenzetu hawa siku hizi ni dakika sufuri tuu kama kuna jambo limetokea wanatuhabarisha mara moja nasisi tuliobeba majumu yakuchukuwa hatua basi tuna chukua hatua lakini siyo kwa mabaya tuu hata kwa mazuri pia nishuku tena kipekee kwa mkoa Kagera vyombo vya habari vyote tunafanya navyo kazi vizuri tuna Redio nyingi ambazo zimekuwa zikitusaidia kutupa hata muda wakuelezea mambo yetu ya msingi kwa jamii kwenye vipindi vyao kwa hiyo hata nyie wadau wetu tumieni vyombo hivi kuelezea mambo mbalimbali kwa wananchi tuweze kufanikiwa zaidi” amesema Mganga Kaniki

Amefafanua kwamba mpango huo jumuishi una maeneo matano ambayo ni afya, ulinzi na usalama wa mtoto, lishe bora na elimu ya awali sambamba na malezi mazuri kwa mtoto.

Ameongeza kuwa Kagera imetekeleza huduma mbali mbali kwa watoto ikiwemo utoaji wa chanjo kwa watoto wote wanaohusika, kupitia shule za awali,msingi, sekondari na vyuo zimepitiwa kwa ajili ya kuangaliwa afya, makuzi na maendeleo ya mtoto.

Ametoa wito kwa wadau kuendelea kushikamana nakushirikiana katika kuendeleza mapambano ya kuwalea watoto vizuri ili wawe na afya njema zaidi hiyo ikiwa nisehemu ya kutekeleza mpango huo kwa vitendo.

Afisa maendeleo ya jamii kutoka wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia,wanawake na makundi maalumu, Joel Mwakapala amebainisha kuwa serikali imekuwa ikifanya jitihada nyingi zakuhakisha malezi ya watoto kwa wazazi na walezi yanatimizwa ipasavyo kwa malengo ya kuzitatua changamoto zinazowakabili watoto pale wanapokuwa wamekosa malezi bora.

Joel amesema serikali imekuwa ikiandaa miongozo thabiti yenye kuwataka wazazi na walezi kuwajibika ipasavyo katika malezi na makuzi ya watoto hususani mwongozo wa mpango huo jumuishi unaotekelezwa kwa sasa nchi nzima.

Mashirika kadhaa yaliyoshiriki katika kikao hicho cha robo ya mwaka yakiwemo ya HEKIMA, HUMULIZA TADEPA nawengineo wameelezea mengi wanayoyafanya katika jamii kulingana na maeneo waliyojikita nayo ambapo shirika la TADEPA kupitia Abemelek Richard kutoka katika shirika hilo ameelezea kuwa wao mpango huo wameutekeleza kupitia njia kadhaa ikiwemo ya vyombo vya habari.

Abemelek amesema kuwa awali waliandaa mwongozo mahususi ukiwalenga waandishi wa habari ambao waliwapatia baadhi yao kwa madhumuni ya kuwajengea ufanisi wakuweza kuandika na kuripoti kwa ufasaha habari za otoaji elimu kuhusiana na mpango huo ili taarifa zikiifikia jamii ziweze kuwa sahihi nazenye kuleta tija ya uelewa kwa kina.

Hata hivyo ameongeza kwamba kwa kutumia njia hiyo ya vyombo vya habari ambavyo ni Redio, Magazeti,mitandao ya kijamii wameweza kuwafikia jumla ya wananchi (1352) ambao niwalezi na wazazi.

Kitu kingine walichofanikiwa kukitekeleza ni pamoja na kushirikiana na wadau mbalimbali wa serikali kwakutumia matukio yaliyopo kama vikao vya wadau wa lishe na kamati za UKIMWI za wilaya.

Ameyataja mafanikio mengine kuwa katika kipindi hicho nipamoja na huo mwongozo kwa waandishi wahabari jambo ambalo limesadia kuripotiwa kwa habari sahihi na muhimu kwa jamii, kuboresha mahusiano mazuri yakiutendaji baina ya shirika la Tadepa ngazi za serikali na wadau wengine.

“Tangu tulivyoanza kutekeleza huu mradi angarau kuna mabadiliko flani kwenye uelewa wawadau na jamii kuhusu mambo ya ya malezi, makuzi na maendeleo ya wali ya mtoto tunaona kidogo kuna kitu kiasi kinaongezeka ukilinganisha na kipindi tunaanza kutekeleza mpango huu mwaka 2022” amefafanua Abemelek mbele ya wadau.

Aidha amezitaja baadhi ya changamoto hasa hasa kutokuwa na uwezo mkubwa wakifedha ili kuwawezesha kuyafikia maeneo yote, wadau mbalimbali na Serikali na wazazi wengine kwenye familia na sekta kutokuona umuhimu wakutoa vipaumbele kwa malezi na makuzi ya wali ya mtoto badala yake unakuta vipaumbele vyao vinahusika maeneo mengine.

Amehitimisha akitoa ushauri kwa wadau na Serikali kubuni njia nyingine zenye kusaidia kusambaza ujumbe wa elimu ya mpango huo kama yalivyo makusudio ya serikali katika kuhakikisha watoto wanalelewa kwa misingi ya malezi bora bila yakusahua njia ya vyombo vya habari.

Watalaamu ambao ni maafisa lishe na maafisa maendeleo ya jamii kutoka halmashari zote za Mkoa Kagera nao wamewasilisha taarifa mbalimbali kwa namna wanavyoutekeleza mpango huo kwakuzingatia makundi yote ya afya, lishe na ulinzi na usalama kwa watoto wote kuanzia majumbani mpaka shuleni.

Afisa maendeleo ya jamii Mkoa Kagera Issa Mrimi akiwa mwenyeji wa kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Bukoba amewashukuru wadau na Serikali kwa ujumla kufika nakujadili maendeleo ya utekelezaji wa mpango huo ambapo amesisitiza kuwa ushirikiano na kasi ya hali ya juu inahitajika zaidi ili kuendelea kutoa elemu kuhusu malengo ya programu hiyo naiweze kuzaa matokeo chanya kwa watoto na jamii nzima ya Kagera.

Kwa pamoja wadau hao wameadhimia mambo kadhaa watakayoyafanyia kazi katika utekelezaji kwa maana yakupanua wigo zaidi katika kufanikiwa malengo ya mpango huo unawalenga watoto kuanzia miaka 0-8 uliozinduliwa mwaka jana 2022.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!