Home Kitaifa SILAHA AINA YA RIFFLE NA RISASI 39 ZAKAMATWA NA JESHI LA POLISI...

SILAHA AINA YA RIFFLE NA RISASI 39 ZAKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MARA

Na Shomari Binda-Musoma

JESHI la polisi mkoani Mara limefanikiwa kukamata silaha aina ya Riffle na risasi 39 ziluzokuwa zikimilikiwa kinyume cha sheria.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake,kamanda wa polisi mkoa wa Mara, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Salim Morcase amesema kukamatwa kwa silaha na risasi hizo ni mafanikio ya oparesheni ya mwezi julai hadi agosti.

Amesema kumiliki siraha kinyume na utaratibu wa sheria ni kosa na mtuhumiwa aliyekutwa na siraha hizo tayari ameshafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Kamanda Salim amesema licha ya siraha hizo lakini katika kipindi hicho wamefanikiwa kukamata vitu mbalimbali vinavyodhaniwa kuwa vya wizi zikiwemo pikipiki 21.

Licha ya pikipiki hizo zimekamatwa pia laptop 6 aina ya Aceer mali ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa( NIDA) ofisi ya Musoma.

Mali nyingine zilizookolewa ni pamoja na TV aina ya LG,deki 2,computer aina ya Lenovo moja,camera moja aina ya Canon na vifaa vingine.

Katika oparesheni hiyo,jeshi la polisi mkoani Mara limekamata kilogram 45.54 na kete 452 za madawa ya kulevya aina ya bangi kavu na watuhumiwa 23.

Aidha kamanda hiyo amesema.hali ya usalama katika mkoa wa Mara kwa sasa ni shwari na wananchi wanaendelea na shughuli zao za kiuchumi kama kawaida.

Amewashukuru pia Waandishi wa Habari na wananchi kwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi na kufanikisha kuzuia uhalifu na kukamatwa kwa wahalifu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!