Home Kitaifa RAIS WA INDONESIA JOKO WIDODO KUFANYA ZIARA YA SIKU MBILI NCHINI

RAIS WA INDONESIA JOKO WIDODO KUFANYA ZIARA YA SIKU MBILI NCHINI

Magrethy Katengu

RAIS wa Jamhuri ya Indonesia Joko widodo anatarajiwa kufanya ziara ya siku mbili na anatarajiwa juwasili leo Agosti 21, 2023, na atapokelewa rasmi na mwenyeji wake, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Tax akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Dkt. Tax amebainisha kwamba baada ya mapokezi, viongozi hawa watakuwa na mazungumzo ya faragha, na baadaye mazungumzo rasmi.

“Baada ya mazungumzo hayo kutakuwa na hafla ya utiaji saini hati za makubaliano ya ushirikiano kwenye sekta mbalimbali kama afya, nishati, madini, uchumi wa buluu, ushirikiano wa kimataifa, uhamaji na biashara,” amesema Dkt. Tax na kuongeza,

“Mara baada tukio hilo , Mheshimiwa Rais Widodo atatembelea Ofisi ya Ubalozi wa Indonesia uliopo hapa nchini kabla ya kuhitimisha ziara yake na kuondoka nchini,”.

Amebainisha kwamba sio mara ya kwanza Tanzania kuwa na uhusiano kati yake na Indonesia.

“Ikumbukwe Kuwa Mkutano wa Bandung uliofanyika mwaka 1955 ambapo nchi nyingi za Afrika na Asia zilikuwa katika utawala wakikoloni kwa kipindi hicho. Kupitia Mkutano huo nchi hizozilikubaliana kuimarisha ushirikiano ili kujikomboa kutokakatika utawala wa kikoloni, na ulikuwa ndiyo msingi wa kuanzishwa kwa Umoja wa Nchi zisizofungamana na Upande Wowote (Non- Aligned Movement –NAM),” amesema.

Hivyo, Tanzania na Indonesia zikawa na uhusiano wa muda mrefu na wa kihistoria.

Ameeleza katika uwekezaji hadi kufikia mwaka 2023, Indonesia imewekeza nchini miradi ipatayo mitano (5) katika sekta za Kilimo.

Kwamba Mwaka 1996 Indonesia ilianzisha Kituo cha Mafunzo ya Kilimo kwa Wakulima Vijijini (Farmers’ Agriculture and Rural Training Centre-FARTC), kilichopo Mikindo mkoani Morogoro.

Ameeleza Kituo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo mbalimbali kwa wakulima.

Aidha, kwa kuzingatia kuwa, Indonesia imepigahatua kubwa katika kilimo cha zao za mchikichi kutokana na kuwa na mbegu bora ya zao hilo pamoja na teknolojia ya kisasa.

Kwamba ziara ya Rais Widodo nchini itapanua wigo wa ushirikiano katika zao la mchikichi utakaowawezesha wakulima wetu za zao hilo kunufaika na mbegu bora ya mchikichi, na hivyo kuwajengea uwezo na kuongeza uzalishaji wa mafuta ya kula.

Ushirikiano wa Kimataifa Tanzania na Indonesia zina uhusiano wa muda mrefu na wa kihistoria, hivyo katika nyanja za Kimataifa, Waziri Tax amesema tanguvwakati wa harakati za kujikomboa kutoka katika utawala wa kikoloni kama wanachama wa Umoja wa Nchi zisizofungamana na Upande Wowote (Non-Aligned Movement –NAM) ambapo nchi zote mbili ni mwanachama wa umoja huo hadi leo.

“Hivyo nchi zetu zimekuwa zikishirikiana katika masuala mbalimbali ya kimataifa. Ziara hii inatarajiwa kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali kama itakavyoonekana katika Hati za Makubaliano zitakazosainiwa, na matokeo ya mazungumzo kati ya Viongozi wetu yatakayojikita katika diplomasia, biashara, kilimo, uvuvi, elimu, nishati, madini, uchumi wa buluu na uhamiaji. taswira njema ya nchi yetu katika sura ya dunia,” amebainisha Waziri Tax.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!