Na Magrethy Katengu
Wasanii wameshauriwa kutumia fursa zinazojitokeza ikiwemo majukwaa mbalimbali, mikutano midahalo na makongamano kwani huwasaidia kupata fusra ya kupata masoko ya kazi zao wanazozifanya pia kukutana na wadau muhimu.
Akitoa taarifa Jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji Basata Kedmon Mapana juu ya Tanzania kuwa mwenyeji tena wa mkutano wa music ACCES amesema utafanyika Novemba 9 -11 mwaka huu na mwandaaji wa mkutano huo anatokea Afrika kusini wakishirikiana karibu sana na Wizara ya Sanaa tamaduni na michezo pamoja na Baraza la Sanaa
“Mkutano huu utahudhuriwa na mataifa mengi na wameona Tanzania ni mahali sahihi na waliangalia kuwa Watanzani ni wakarimu wanapenda mziki ni nchi yenye amani na usalama huduma. zao ni nzuri ” Dkt. Mapana
Kwa upande Mkurugenzi wa Taasisi ya “Music in Africa Foundation na ACCES Eddie Hatitye ambaye ni muandaaji wa mkutano huo amesema fursa pekee ya muhimu kupatikana masoko ya mziki kupitia fursa hiyo hivyo wasanii wote nchini wakiwemo chipukizi na watafanikiwa kuonyesha vipaji vyao
“Lengo la tamasha hilo ambalo linandaliwa na Taasisi ya Music in Africa kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Tanzania ni kuwasaidia wanamuziki kutambuana na kuonyesha uwezo wao wa kuimba pamoja nakufundishwa namna ya kuchangamkia fursa za masoko” amesema Eddie
Tamasha hilo la ACCES linatarajiwa kuhudhuriwa na wadau wa muziki zaidi ya 1000 kutoka zaidi ya mataifa 50 duniani ambapo kwa Tanzania linafanyika kwa mara ya pili pia mwaka jana lilifanyika Novemba 24-26, 2022 jijini Dar es Salaam
Naye Mratibu wa Mkutano huo upande wa Tanzania Mandolin Kahindi amesema kwa mwaka jana walivyofanya walifanikiwa vizuri sana hivyo mkutano huo unakuwa wa tofauti unakuwa na wadau muhimu ukiwemo wanaonunua mziki kwa njia ya mitandao wanakuwepo ambapo hao wadau kama hao huwezi kukutana nao peke yao hivyo uhudhirie na
Aidha tunawakaribisha wote kuhudhiria ni bure kabisa watangazaji wenye studuo wanamziki wote kwani mchana tutafanyia JNCC Mwalimu Nyerere Dar es salaam Usiku tutatafuta eneo kwanu itakuwa ni kuobesha kazi zao majukwaani kama alivyojitokeza Sholo Mwamba akapata fursa ya kwenda nje ya nchi usiache ni fursa adhimu.