Na Shomari Binda-Musoma
MENEJA wa kampuni ya Froza Microfinance Company Limited,Mbio Mushi ,amesema suala la elimu kwa wajasiliamali ni muhimu ili kuwezesha biashara kukua.
Kauli hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na Mzawa Blog kwenye ofisi za kampuni hiyo zilizopo barabara ya Serengeti mjini hapa.
Amesema suala la elimu katika kumuinua mjasiliamali lina nafasi kubwa na si kumuwezesha fedha bila kumpa elimu.
Mbio amesema kampuni ya Froza inao wataalamu wawezeshaji ambao huitoa elimu hiyo bure ili kumfanya mjasiliamali anapokopa fedha aweze kufanya marejesho.
Amesema unaweza kufikia hatua ya kumtolea lawama mjasiliamali kuto kurejesha fedha wakati hukumpatia elimu kabla ya kumuwezesha fedha.
Meneja huyo amesema tangu kuanza shughuli za uwezeshaji fedha kwa wajasiliamali mjini Musoma wamewafikia zaidi ya wajasiliamali 50.
“Sisi elimu kwa wajasiliamali ni kitu cha kipaumbele ili kuwawezesha kuendesha biashara bila kuyumba na kufanya marejesho”
“Tunashukuru wajasiliamali tuliokuwa nao wanaendelea vizuri na tunawakaribisha wengine watufikie tuweze kuwawezesha elimu ya ujasiliamali na kupata mikopo”,amesema Mbio.
Amesema wajasiliamali mjini Musoma bado wanayo nafasi ya kupatiwa elimu kupitia kampuni ya Froza ili kuinua biashara zao na kuwa wakubwa.