Home Kitaifa MUHONGO ACHANGIA MIFUKO 200 YA SARUJI KUUNGA MKONO WANAKIJIJI UJENZI WA ZAHANATI

MUHONGO ACHANGIA MIFUKO 200 YA SARUJI KUUNGA MKONO WANAKIJIJI UJENZI WA ZAHANATI

Na Shomari Binda-Musoma

MBUNGE wa jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo amechangia mifuko 200 ya saruji kuunga mkono wananchi wa Kijiji cha Chimati walioamua kufufua ujenzi wa zahanati ya Kijiji.

Kijiji cha Chimati cha Musoma Vijijini ni moja ya vijiji vitatu vya Kata ya Makojo vikiwa ni pamoja na vijiji vya Chitare na Makojo.

Kwa muda wa miaka mingi Kata hiyo yenye vijiji vitatu ilikuwa inahudumiwa na zahanati moja ya Kjiji cha Chitare.

Utoaji wa Huduma za Afya kwenye Kata ya Makojo inaenda kubadilika kwa maboresho makubwa kikiwemo kituo cha afya cha Kata kilichojengwa Kijiji cha Makojo.

Kijiji cha Chimati kimeamua kufufua mradi wa ujenzi wa zahanati yao ulioanza mwaka 2018 na kusimama hadi leo unapoendelezwa.

Mbunge wa jimbo hilo, Prof Sospeter Muhongo, ameungana tena na wananchi wa Kijiji cha Chimati kuendelea na ujenzi wa zahanati ya Kijiji chao.

Ujenzi ulipoanza mwaka 2018 mbunge huyo alianza kutoa michango yake kwa kuchangia saruji mifuko 50 na kuwapongeza kwa kuamua kufufua ujenzi huo.

Muhongo alitembelea zahanati hiyo aliambatana na Kamati ya Siasa ya CCM ya Wilaya ya Musoma vijijini na kuendesha harambee kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya Kijiji hicho.

Kwenye harambee hiyo,wanakijiji na wazaliwa wa hapo wmechangia mifuko 123, Kamati ya Siasa (CCM) ya Wilaya saruji mifuko 25 huku mbunge wa jimbo akichangia mifuko 200.

Aidha mbunge wa jimbo alipokea kero na matatizo yanayowakabili wananchi na kuyatolea majibu ambayo waliridhika nayo.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Musoma vijijini Denis Ekwabi na Katibu wa Chama hicho Valentine Maganga walijibu maswali yaliyoelekezwa kwenye chama na kutoa elimu na ufafanuzi kwa masuala mengine yaliyoulizwa.

Jimbo la Musoma Vijijini linaendelea kuboresha utoaji wa huduma za afya na takwimu za sasa zinaonywsha hospital yenye hadhi ya wilaya:
1 imeanza kutoa huduma

Pia vituo vya afya 6 vinatoa huduma
na 2 vinatoa huduma kwa hadhi ya zahanati
2 ni vipya vinasubiri kufunguliwa huku zahanati zaidi ya 40 zikitoa huduma.

Niwashukuru sana wanakijji wa Chimati kwa kuamua kufufua ujenzi wa zahanati hii na mimi ntawaunga mkono hadi ikamilike” amesema Muhongo.

Katika Kijiji hicho pia tenki la maji la ujazo wa lita 75,000 linakamilishwa ujenzi kwaajili ya maji ya bomba ya Kijiji hicho.

Wananchi na Viongozi wote wa jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kuishuruku serikali chini ya uongozi mzuri wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutoa fedha za miradi mbalimbali ikiwemo ya sekta ya afya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!