Home Biashara VIJANA WABUNIFU WAMEIOMBA SERIKALI KUWAWEZESHA MITAJI

VIJANA WABUNIFU WAMEIOMBA SERIKALI KUWAWEZESHA MITAJI

Vijana wabunifu wameiomba serikali kuwawezesha mitaji itakayoweza kukuza mitaji yao

hayo yamesemwa na Bwana Ramadhani Mohamed Sengerema katika Maonesho ya Nanenane yanaendelea katika Viwanja vya nyamongoro “sisi kama Vijana tuna Imani na Serikali iliyopo Madarakani hivyo tunaiomba iweze kutuwezesha Mitaji ya kutusaidia katika kukuza uzalishaji wetu”

Mohamed alisema uwezo wao Kwa Sasa wanazalisha Majiko 10 ambapo Majiko yanaisha Kwa siku Moja hivyo endapo serikali itawasaidia watazalisha majiiko1000 ndani ya wiki moja

tunaiomba serikali itusaidie Kwa Sababu hii kazi ya kuzalisha Majiko 10 inaweza kutupelekea kukata Tamaaa kazi zetu za kutengeneza Majiko inatusaidia Sisi na Familia zetu inafika muda tunapigiwa simu za watu wa Mikoani kulingana na Ubora wa Majiko yetu yalivyo ni imara na Mazuri” alisema Mkurugezi uyo

Naye Halima Said Mkazi wa Kisesa Ambae ni miongoni mwao watu ambao wameshatumia Majiko hayo alisema ni Majiko Imara ya Yanadumu Muda Mrefu siyo kama Majiko yaliyozoeleka Mtaani alisema Halima Vijana wengi wanapoitimu wanatarajia kuajiliwa lakini uyu Mohamed amekuwa ni kijana Wa Tofauti Ambae ameweza kujiajiri na kuajili Vijana wenzake ikiwa ni
Pamoja na kuisaidia serikali kutatua Changamoto ya Ajira
Vijana hao wameiomba serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwawezesha Ili waweze kuongeza uzalishaji wa Majiko kwani kwa sasa wanatengeneza kiwango kidogo ambacho hakikidhi Mahitaji ya soko lao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!