Home Biashara MHE. DKT.KIJAJI AIAGIZA MENEJIMENTI YA KIWANDA CHA SUKARI CHA MKULAZI KUKAMILISHA UJENZI...

MHE. DKT.KIJAJI AIAGIZA MENEJIMENTI YA KIWANDA CHA SUKARI CHA MKULAZI KUKAMILISHA UJENZI WA KIWANDA HICHO

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameiagiza menejimenti ya kiwanda cha sukari cha Mkulazi Holding Company Limited (MHCL) ambacho ni kiwanda cha ubia kati ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na jeshi la magereza Tanzania kuanza uzalishaji ifikapo mwezi septemba 2023.

Mhe. Dkt. Kijaji ameyasema hayo tarehe 11 Agosti, 2023 alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha sukari na miundombinu ya umwagiliaji katika shamba la Mbigiri.
Mhe. Dkt. Kijaji ameongeza kuwa chini ya uongozi wa rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia mpango wa kuboresha mazingira ya biashara ambapo uzalishaji wa sukari nchini umeongezeka na ifikapo 2025 nakisi ya sukari nchini haitakuwepo tena.

Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi kimefunga mfumo mmoja wa kuzalisha sukari ya viwandani na ni mwanzo mzuri na tunatarajia ifikapo mwaka 2030 hatutaagiza tena sukari nje ya nchi, sisi tuliopewa dhamana ya kusimamia sekta hii ndio jukumu letu kuhakikisha lengo linafikiwa. Amesema Mhe. Dkt. Kijaji.

Vilevile Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima amesema kuwa kiwanda hiki cha Mkulazi ni kiwanda cha kimkakati na kinamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 hivyo kukasirishwa na kuchelewa kuanza kazi kwa wakati.

Mhe. Malima ameongeza kuwa kazi kubwa ya mkoa wake ni kufuatilia kwa karibu kukamilika kwa kiwanda hicho na hakuna makubaliano mengine yatakayofanyika isipokuwa kikamilike kwa haraka na kianze kazi ifikapo mwezi septemba mwaka huu.

Naye Bw. Lusomyo Buzingo ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za udhibiti akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya sukari amesema kuwa kiwanda hiki kinaenda kuzalisha tani elfu hamsini (50,000) na baadaye kuongezeka hadi tani elfu sabini na tano na kwa nchini kwetu hakuna kiwanda kinachozalisha sukari ya viwandani na kiasi chote takribani tani laki mbili na hamsini tunaagiza kutoka nje ya nchi hivyo kuja kwa kiwanda hiki utaenda kuongeza kapu la uzalishaji na kupunguza nakisi ya sukari na tutapunguza matumizi ya fedha za kigeni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!