New Delhi, India*
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amekutana na kuzungumza na Ms. Harsha Bangari, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim ya India
Kikao hicho kimefanyika New Delhi, India ambapo Mh. Aweso kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameishukuru Benki ya Exim ya India kwa kushirikiana na Tanzania hususani katika Sekta ya Maji kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maji ikiwemo mradi mkubwa wa maji wa Tabora-Igunga-Nzega na Tinde-Shelui.
Aidha, amemshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Exim ya India kwa kuendelea na ushirikiano katika utekelezaji mradi wa maji wa kihistoria wa Miji 28 ambapo Benki hiyo imetoa zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 500.
Katika hatua Nyingine, Waziri Aweso ameiomba benki hiyo kuendelea kushirikiana na kuiunga mkono kwa rasilimali fedha Tanzania katika kutekeleza miradi ya maji ya kimkakati na kutoa wasilisho lenye mapendekezo ya maeneo muhimu kwa sasa na kusisitiza kwa pamoja kuendelea kudumisha mashirikiano baina ya Tanzania na India katika sekta muhimu ya Maji.
Katika hatua nyingine kwenye kikao hicho Mhe. Aweso amewasilisha umuhimu na maono ya dhati ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwezesha upatikanaji wa Fedha kwa Tanzania katika katika kufanikisha jiji la Dodoma kufanikisha mradi wa maji kutoa Ziwa Victoria kutokana na ongezeko la watu na mradi wa Rufiji – Dar es salaam ikiwa ni hatua ya kumaliza changamoto ya huduma ya maji katika majiji hayo.