Home Afya TFNC WAAJIRI TOENI LIKIZO SIKU 84 AU 100 KWA MAMA MJAMZITO NA...

TFNC WAAJIRI TOENI LIKIZO SIKU 84 AU 100 KWA MAMA MJAMZITO NA BABA SIKU 3 AU 4

Na Magrethy Katengu

Taasisi ya Chakula na Lishe TFNC imewaimomba Waajiri kutoaa likizo Kwa mama mjamzito aliyejifungua mtoto mmoja siku 84 na zaidi ya mtoto mmoja siku 100 huku baba akipewa likizo siku tatu na endapo akifiwa na mtoto au mwenza wake siku 4

Wito huo umetolewa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji TFNC Dkt Germanya Leyna wakati akifungua semima kwa waandishi wa habari ambapo amesema ni haki zinazomwezesha mwanamke mwajiriwa kutimiz majukumu yake ya uzazi na kufanya kazi au kuzalisha bila kubaguliwa au kubugudhiwa au kupotezea ajira

“Likizi ya uzazi ni Moja ya haki ya uzazi humpa mama muda wa kumwezesha kutoa matunzo muhimu kwa mtoto katika miezi ya mwanzo ya maisha yake ikiwa ni pamoja na kumnuonyesha mtoto maziwa ya mwazo kwa wakati pasipo kumpatia chochote ” amesema Mkurugenzi

Sanjari na hayo amesema mama ana hakinya kuchukua likizo wiki ya nne kabla ya kujifungua na iwapo ana uthibitisho wa daktari kwana ana matatizo yotote ya kiafya yeye au mtoto apeleke cheti Cha daktari kwa mwajiri wake ili aongezewe likizo na mwajiri asimfukuze kazi mwajiriwa wake sababu ya matatizo kama yeye hajataka kwani anaweza kumsababishia msongo wa mawazo hivyo atumie hekima na busara matatizo yanaisha .

Naye Mwamuzi Mwandamizi Ofisi ya Waziri Mkuu kazi,ajira,vijana na watu wenye ulemavu Yohana Maswe Mtoa maada katika semiana hiyo mwajiri hatakiwi kumpatia mwanamke mwenye mimba au kunyonyesha kazi ngumu mfano anafanya kazi tanesko kumpangia apande juu ya kufunga nyaya za umeme au kama ni Muendesha magari kumpangia kuendesha gari safari za usiku au safari za mbali hivyo anashauriwa kutumia hekima na busara kwa mwajiriwa wake ili kusaidia afya yake.

Sambamba na hayo Mwandamizi huyo amebainisha sheria pia inamtaka mwajiri kumpa likizo baba wa mtoto aliyezaliwa siku tatu wiki Moja ya mwanzo bila kujali idadi ya watoto kwani likizo hiyo inamsaidia baba kumuhudumia mama na mtoto kujenga msingi mzuri kumlisha mtoto pia kutafuta mahitaji ya kifamilia endapo mama amelazwa hospitali lazima awe karibu naye .

Baba mtoto aliyebarikiwa kupata mtoto zaidi ya mmoja anatakiwa kupatiwa likizo ya siku 4 yenye malipo na wakati wa kuuguliwa au kifo cha mtoto au mwenzi wake atoe taarifa kwa mwajiri wake au kupeleka cheti Cha daktari hekima itumike asifukuzwe kazi bali apewe likizo kulingana na tatizo alilopata na mwanamke naye hivyo hivyo kama siku zake za likizo zimeisha “ amesema Masawe

Aidha Wito umetolewa kwa waajiri kuwa likizo kwa mwajiri Ina faida kwa Taifa inamwezesha mwanamke aliyeajiriwa kumpa mtoto matunzo muhimu katika miezi yake ya mwanzo ya maisha yake

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!