Na Magrethy Katengu
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) yatangaza ushirikiano na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) katika uendeshaji wa Akaunti ya dhamana (Trust Account) ili kusaidia uimarisha na usimamizi wa sekta ya bima nchini ili kuendana na matakwa ya kisheria na udhibiti yaliyowekwa na TIRA.
Ushirikiano huo umewekwa wazi rasmi leo jijini Dar es Salaam na Kamishna wa TIRA Baghayo Saqware wakati wa hafla fupi iliyoambatana sambamba na mafunzo kwa wadau mbalimbali wa sekta ya bima nchini wakiwemo viongozi waandamizi kutoka TIRA, Benki ya NBC pamoja na wawakilishi wa makampuni ya bima nchini na wakurugenzi na maofisa wa fedha wa kampuni hizo ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo .
“Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) leo tumeanzisha mashirikiano na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) katika kuhakikisha kuwa Kampuni za bima hapa nchini zinatumia akaunti ya dhamana katika mabenki ili kuepusha changamoto ya kampuni hizo kutumia fedha bila ruhusa ya Kamishna wa Bima” amesema Kamishna
Hata hivyo amewahakikishia watanzania kuwa kampuni za bima wanazozisimamia zina ukwasi wakutosha na zinaweza kulipa madai ya fidia ya kwa watumiaji wa bima
“Hapo awali kulikuwa na changamoto ndogo ambapo kampuni za bima zilikuwa na kiwango cha fedha katika Benki ya Tanzania (BoT) lakini kiwango hicho huwekwa kwenye hati fungani na zinapoiva zinarudi katika akaunti ya kampuni ya bima hivyo tukawa tunapata changamoto ya baadhi ya kampuni hizi kutumia fedha hizo bila ruhusa ya Kamishna wa Bima” Amesema Dkt. Saqware
Sambamba na hayo amesem ili kuondoa changamoto hiyo wameanzisha akaunti ya dhamana ambayo tunaipa masharti na benki hivyo Benki ya NBC imetimiza masharti hayo ya kufungua akaunti hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki ya NBC Theobald Sabi amesema wamefanikiwa kutimiza matakwa ya masharti yaliyowekwa na TIRA hivyo itawezesha watu wa bima kulindwa hivyo wanategemea kuwapa wateja wao huduma nzuri kupitia mfumo wa kieletroniki ambapo Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania itakuwa inafuatilia mwenendo huo.
“Sisi NBC ni benki ambayo imekuwepo kwa miongo mitano hivyo tunayo furaha kutoa mafunzo haya kwa wadau wa bima pia Benki ya NBC tumejipanga vyema katika kutoa ushauri wa uwekezaji kupitia Idara yetu ya Hazina na Masoko ya Mitaji hivyo nitoe wito kwa makampuni ya bima nchini kuzingatia taratibu zilizowekwa” Amesema Bw. Sabi.
Pi Mkurugenzi wa Usimamizi wa TIRA Bw. Abubakar Ndwata amesema chimbuko la Akaunti hiyo ya Dhamana ya Bima ni Kanuni ya Bima ya mwaka 2009 inayozitaka Kampuni za Bima kuweka Amana za Usalama angalau 50% ya kiwango cha chini cha mtaji halisi wa kampuni husika ya bima.
Ndwata amesema TIRA kwa kushirikiana na Chama cha Makampuni ya Bima Tanzania (ATI), walikubaliana kuandaa Mwongozo wa Uwekezaji wa Usimamizi wa Ukwasi ambao pia ulielekeza uanzishwaji wa Akaunti ya Dhamana ya Akiba kupitia benki za biashara ili kuondokana na tatizo la changamoto ya kimtaji au kushindwa kulipa fidia za madai ya wateja wake.