Hospital ya Rufaa ya Benjamin Mkapa Dodoma imesema Kiasi cha Shilingi Milioni 6 hadi 10 gharama ambazo zinatumika katika huduma ya upandikizaji uume.
Akizungumza Agosti 1 Jijini Dodoma wakati akielezea vipaumbele vya bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/24 Mkurugenzi wa Hospital hiyo Dkt. Alphonce Chandika amesema huduma hiyo imeanzishwa baada ya kubaini kuwa kuna changamoto kubwa ambayo imewafanya waganga wa kienyeji kupita mitaani na dawa zinazodaiwa kutibu tatizo hilo.
Akizungumza maendeleo ya wanaume wawili waliofanyiwa upandikizwaji amesema habari njema kutoka kwa wanaume hao, mambo yamekuwa mazuri na kwamba hivi sasa wako katika mkakati wa kupanua wigo wa huduma ili kuifanya ipatikane kwa kila anayehitaji
Pia. Dk Chandika amesema katika mwaka wa fedha 2023/24 wametengewa Sh bilioni 64.52 na kwamba Shilingi bilioni 18.62 zitakwenda katika miradi ya maendeleo ili kuendelea kuwapunguzia wananchi adha ya kusafiri mbali kupata matibabu.
Ameitaja miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa jengo la saratani, jengo la matibabu ya moyo na kifua kwa watoto na watu wazima na kituo cha upandikizi wa figo.