Home Kitaifa Maboresho muhimu kuepuka soko kuchukuliwa na Nchi Jirani

Maboresho muhimu kuepuka soko kuchukuliwa na Nchi Jirani

KUPUNGUA uwezo wa kupitisha shehena ya mizigo bandari ya Dar essalaam kwenda mataifa mengine kutasababisha washindani wa usafirishaji na Tanzania kuchukua fursa hiyo na hivyo kuathiri ukuaji wa uchumi.

Hayo yamebainishwa jana Jijini Mwanza na Naibu Waziri wa ujenzi na uchukuzi Atupele Mwakibete akisema kuwa mwaka jana mizigo ya shehena tani milioni 8.3 ndo zilipitia katika bandari hiyo badala ya tani milioni 60.

“Mataifa hayo yenye kupitisha mizigo hayakuweza kupitishia mizigo kwetu kwa sababu ya kuepuka changamoto zilizopo kwenye bandari yetu” alisema Mwakibete.

Alisema ni jukumu la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) pamoja na serikali kuharakisha maboresho ya eneo hilo ili mataifa yenye bandari yasiweze kuchukua soko hilo mhimu kwa usitawi wa taifa.

Mwakibete alisema kuwa mataifa kama vile Zambia, Malawi, Burundi Zimbabwe, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Uganda kuwa miongoni mwa nchi zinazotegema kupitishia mizigo yao hapo.

Kwa sasa nchi zenye bandari shindani na Dar es salaam ni Mombasa nchini Kenya, Durban Afrika Kusini ambazo kwa pamoja upakuaji wa shehena hufanyika kwa siku moja huku hapa ni siku tano.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilayani Kwimba Sabana Salinja alisema jitihada ambazo zimeanza kuchukuliwa kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwenye bandari hiyo kutasaidia kuepusha taifa kupoteza fursa hiyo ya uhakika katika kuingiza pato la taifa.

Aliwaomba watanzania kuamini viongozi wao kwani wanao wanasheria wazalendo wanaofahamu mikataba hivyo hawawezi kukubali kuliingiza taifa katika masuala mabaya.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Geita ambaye pia ni Diwani ya Kata ya Butobela Charles Kazungu alisema juhudi ambazo zinaonekana za ujenzi wa vyumba vya madarasa, miundo mbinu ya afya, barabara nchini kote bila ya kuchangishwa wananchi fedha ni dhamira nzuri kwa taifa kuondoa mzigo kwa watu wake.

Hivyo aliomba wananchi kuona jitihada za serikali kurekebisha maeneo ambayo hayakuwa na tija ziweze kuchangia pato la taifa kuwa ni hitaji mhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!